Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile, leo, anatarajia
kuwasomea hoja za awali Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema na mkewe,
Neema katika kesi inayowakabili ya kumtukana Mkuu wa mkoa huo, Mrisho
Gambo.
Hoja hizo ilikuwa wasomewe Novemba 15, 2016 lakini zilikwama
kusomwa kutokana na Lema kuugua ghafla na Wakili wa Serikali, Elizabeth
Swai kumuomba hakimu kutumia busara ya Mahakama kuisogeza mbele kesi
hiyo kutokana na hali ya mbunge huyo.
Lema bado anasota rumande kwa siku
76 tangu Novemba 2, mwaka jana baada ya kukosa dhamana katika kesi
inayomkabili ya tuhuma za kutumia lugha ya uchochezi dhidi ya Rais John
Magufuli.
Kutokana na sababu hiyo, Hakimu Rwezile pia
aliahirisha kesi ya kuhamasisha maandamano ya Ukuta inayomkabili mbunge
huyo na ile ya kumtumia ujumbe mfupi wa maneno Gambo unaodaiwa kuwa na
matusi hadi leo.
Katika kesi ya kuhamasisha maandamano inayomkabili Lema
peke yake, shahidi ambaye ni Mkuu wa Makosa ya Jinai Mkoa (RCO) wa
Arusha, George Katabazi ataanza kutoa ushahidi wake ambao ilikuwa atoe
Novemba 15.
Awali, upande wa Jamhuri ulidai utakuwa na mashahidi
watano katika kesi ya kuhamaisha maandamano na upelelezi umekamilika.
Mashahidi wengine ni ASP Damas Masawe ambaye ni (OCCID), Inspekta Adam Nyamiti, WP 6826 DC Esta Yohana na Ezekiel Denis Kwayu kutoka kitengo cha Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
Mashahidi wengine ni ASP Damas Masawe ambaye ni (OCCID), Inspekta Adam Nyamiti, WP 6826 DC Esta Yohana na Ezekiel Denis Kwayu kutoka kitengo cha Upelelezi Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam.
Kwa
upande wa kesi ya Lema na mkewe ya kumtumia ujumbe wa matusi Gambo,
itaanza kusomwa maelezo ya awali ambayo nayo itakuwa tayari kwa kuanza
kusikiliza baada ya upelelezi kukamilika.