Aliyekuwa Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa katika Sekretarieti ya Chama cha ACT-Wazalendo, Habibu Mchange, amejiondoa uanachama wa chama hicho na kujiweka kando na siasa.
Taarifa
ya uamuzi huo wa Mchange ilisambazwa jana katika mitandao ya kijamii,
ikionyesha kuandikwa naye huku ikiambatanishwa na namba yake ya simu.
Katika
andiko hilo, Mchange aliyewahi kuwa mwanachama wa Chadema kabla
hajahamia ACT Wazalendo, alisema aliamua kujitoa rasmi katika ushiriki
wa aina yoyote ya siasa ili apate muda zaidi wa kusimamia shughuli zake
za kijasiriamali.
Mchange alisema ameamua kujiengua na siasa ili kutoa fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa.
“Kwa
moyo mkunjufu kabisa na kwa mapenzi mema na taifa langu, ninathibitisha
kwamba nimejitoa rasmi katika ushiriki wa aina yote ya siasa ili nipate
muda mwingi zaidi kufanya na kusimamia shughuli zangu za kijasiriamali
zinazonitaka nitoe fursa na huduma sawa kwa viongozi na wanachama wa
vyama vyote vya siasa,” alisema Mchange.
Alisema
kutokana na uamuzi huo ambao aliomba uheshimiwe, lolote atakalolifanya
lisihusishwe na chama bali iwe ni msimamo wake mwenyewe kama mtu huru
asiye na chama.
“Ninafahamu
kuwa mwanachama wa chama cha siasa ni haki yangu ya kikatiba, lakini
nimeamua kuihifadhi kwa sasa mpaka hapo nitakapoona inafaa kufanya
vinginevyo. Ninawatakia kila la heri waliokuwa wanachama wenzangu wa ACT
Wazalendo katika kuyafikia malengo ya msingi ya uanzishwaji wa chama
hicho,” alisema Mchange.
Mchange
alisema kujiondoa kwake kusihesabiwe kama sehemu ya kukwamisha au
kurudisha nyuma matarajio na au malengo ya chama hicho bali ichukuliwe
kama chachu ya kufika mbali.
“Msivunjike
moyo, msirumbane, pendaneni, heshimianeni na shikamaneni ili mfikie
lengo. Nitabaki na kuendelea kuwa ndugu yenu, rafiki na swahiba. Zaidi
Mtanzania mwenzenu. Tutaendelea kushirikiana katika mambo yote ya
kijamii na kimaisha yasiyohusiana na mlengo wa kiitikadi wa kisiasa,”
alisema Mchange.
Mchange
alishika nafasi mbalimbali katika chama hicho ikiwamo Katibu wa Mipango
na Mikakati, Mjumbe wa Kamati Kuu, Mjumbe wa Halmashauri Kuu na Mjumbe
wa Mkutano Mkuu.
Mchange
anakuwa mwanasiasa wa tatu kuondoka ACT-Wazalendo mwaka huu baada ya
aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho, Samson Mwigamba kuachia nafasi
yake na kwenda masomoni nchini Kenya, Aprili mwaka huu.
Miezi
michache baadaye, Novemba mwaka huu mwanasiasa Moses Machali naye
alitangaza kujiondoa rasmi chama hicho na kuunga mkono jitihada
zinazofanywa na Rais Dk. John Magufuli.
Machali
aliwahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini kupitia Chama cha NCCR-Mageuzi
Kutoka kwa HABIBU MCHANGE.
TAARIFA KWA UMMA
--------------------------------------
YAH:- KUJIVUA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO NA KUTOSHIRIKI SIASA....
See More
TAARIFA KWA UMMA
--------------------------------------
YAH:- KUJIVUA UANACHAMA WA ACT WAZALENDO NA KUTOSHIRIKI SIASA....
See More
kabla ya mwaka jana kushindwa kutetea jimbo lake kupitia ACT-Wazalendo.