Aliyekuwa Waziri na Mbunge wa Jimbo la Bunda, Stephen Wasira, amesema kuwa taarifa zilizozagaa kwenye mitandao ya kijamii zikidai kuwa ameteuliwa kuwa msemaji wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) sio za kweli.
Taarifa
hiyo imedai kuwa Wasira ameteuliwa kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na
Christopher Ole Sendeka aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa Mkuu wa Mkoa
wa Njombe huku nafasi ya mweka hazina na Naibu Katibu Zanzibar zikidaiwa
kupata viongozi wapya.
Wasira
amesema kuwa taarifa hizo sio za kweli na ni uzushi tu wa watu ambao
wana nia mbaya na hawamtakii mema.Pia CCM kupitia ukurasa wao wa Twitter alikanusha taarifa hizo
“Zipuuzeni
hizo taarifa, hakuna kitu kama hicho, nmepigiwa simu na watu wengi sana
wanaulizia suala hili. Na sijui kuna ajenda gani nyuma ya hawa
waliozusha” Amesema Wasira.
Wasira
amekuwa mwanachama wa CCM kwa muda mrefu huku akishika nyadhifa mbali
mbali, ingawa mwaka 1995,alikihama chanma hicho na kujiunga na
NCCR-Mageuzi baada ya kuangushwa kwenye kura za maoni za ndani ya CCM na
Jaji Joseph Sinde Warioba.