Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa
habari juu ya amempongeza Makonda kwa kutafuta vijana wanasheria na
kuwapeleka katika kila Wilaya ya Dar es salaam ilikuweza kuwaidia
wananchi wanyonge katika masuala ya kisheria, leo jijini Dar es Salaam.
Kukia ni Mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda. Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu
wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda akizungumza na waandishi wa
habari juu ya ujenzi wa Mahakama utapunguza mzigo mkubwa kwa Serikali
na itasaidi wakazi Nje ya Dar es salaam na Ndani katika kupata Haki Zao
za kisheria kwa haraka leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa
Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe
Waziri
wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe akisanikitambu cha wageni
katika ofisi ya mkuu wa mkoa leo jijini Dar es Salaam.
Waziri
wa Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya
pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda Katibu
Mkuu wa Sheria na Katiba, Profesa Sifuni Mchome, Naibu Katibu Mkuu wa
Sheria na Katika, Amon Mpanju
MKUU
wa Mkoa Wa Dar es salaam Paul Makonda ameahidi kuanza Ujenzi wa
Mahakama 20 za Mwanzo katika Mkoa wa Dar es salaam ili kupunguza
msongamano wa mahabusu katika vituo vya polisi na Magereza.
Hayo
ameyasema leo Makonda wakati alipotembelewa na Waziri wa Katiba na
Sheria, Harrison Mwakyembe, ofisini kwake, amesema ujenzi huo wa
Mahakama utapunguza mzigo kwa Serikali na itasaidia wakazi walio nje
kidogo jiji la Dar es salaam kuweza kupata haki kwa wakati.
Makonda alitoa wito kwa badhi ya Wadau mbalimbali kujitokeza ili kusaidia ujenzi wa Mahakama hizo, Amesema mtu yeyote atakaye kwenda kinyume na sheria hatakama alisaidia kujenga Mahakama, sheria itafata mkondo wake.
Nae
Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Harrison Mwakyembe amempongeza Makonda
kwa kutafuta vijana wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya katika
jiji la Dar es salaam ilikuweza kuwaidia wananchi kuwanyonge kupata
haki katika masuala ya kisheria.
"
Sisi kama Wizara tunampongeza Mkuu wa Mkoa kwa kuwatafuta vijana
mbambali wanasheria na kuwapeleka katika kila Wilaya ilikuweza
kuwasaidia wananchi hawa kupata msaada wa kisheria ilikupunguza uonevu
kwa baadhi ya watu".amesema Mwakyembe.
Amesema
katika ujenzi huo wa Mahakama za mwanzo kutawasaidia wakazi mbalimbali
wa jiji la Dar es salaam kuwa na uhakika wa kupata haki kwa wakati
mwafaka na kupunguza baadhi ya migogoro katika jamii na serikali..