Chama
cha Wananchi (CUF), kimetakiwa kuacha kufuatilia na kuhoji uhalali wa
kikao cha Kamati Kuu (CC) ya Chama cha Mapinduzi( CCM) kufanya vikao
vyake Ikulu kwa madai kuwa kufanya hivyo ni kutumia rasilimali za umma
kwa maslahi ya chama.
Aidha
taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM), Shaka Hamdu Shaka ,kwa vyombo vya habari jijini Dar es salaam,
imesema hoja hiyo iliyotolewa na kiongozi wa CUF, Mbarara Maharagande
kushutumu hatua hiyo haina mashiko.
“UVCCM
tunamwambia mwanasiasa huyo, amekwenda kombo, hajui kulinganisha wala
kutofautisha mambo, alichokisema ni porojo tu na hiyo taarifa
aliyoiandika kwa umma haina mantiki, haikuwa na kichwa wala
miguu,kiufupi haikueleweka na kufahamika alichokusudia kukisema”amesema Shaka.
Shaka
amesema kuwa Viongozi mbalimbali wa Upinzani wamekuwa wakialikwa Ikulu
na kutumia rasilimia hizo ikiwemo kuandaliwa chakula na vinywaji.
Aidha,
amemtaka Maharagande kutumia muda na rasilimali za CUF kutatua mgogoro
uliokigubika chama chao na kuwafanya viongozi wao kutokaa meza moja.