Serikali
ya China imetoa ufadhili wa ujenzi wa uwanja wa Michezo kwa shule ya
msingi Msoga iliyopo halmashauri ya wilaya ya Chalinze….
Akizungumza
katika hafla ya kuoneshwa eneo patakapojengwa uwanja huo Rais mstaafu
wa awamu ya nne Dkt Jakaya Kikwete ameishukuru serikali ya China kwa
msaada huo kwakuwa Michezo ni Kitu muhimu kwa watoto huku akitoa rai kwa
halmashauri ya chalinze kulinda eneo hilo.
Kwaupande
wake mwakilishi wa balozi wa China amesema kuwa China inajivunia
uhusiano mwema uliopo kati ya China na Tanzania,na watahakikisha
wanajenga uwanja huo kwa wakati ili kuwapa fursa watoto kufurahia
michezo.
Nae
Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete ametoa rai kwa wananchi wake
kuhakikisha eneo lililotengwa linalindwa ili dhamira ya china kujenga
uwanja huo itimie
Ufadhili
wa ujenzi wa uwanja huo wa michezo kwa watoto wa Msoga ni muendelezo wa
ufadhili wa China katika kijiji cha Msoga baada ya kujenga shule ya
msingi Msoga.