test

Alhamisi, 22 Desemba 2016

Shahidi wa pili atoa ushahidi Kesi ya Tundu Lissu.......Neno ‘dikteta uchwara’ Latikisa


Kesi ya uchochezi dhidi ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu jana imeendelea katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam ambapo upande wa Mashtaka umetoa ushahidi wa pili.

Lissu anakabiliwa na mashtaka ya kutoa kauli za kichochezi na maudhi dhidi ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli.

Shahidi huyo wa pili aliyetambulishwa kama ASP Kimweri, alisema kauli ya Lissu aliyoitoa June 28 mwaka huu kuhusu ‘Dikteta uchwara’, ililenga katika kufanya uchochezi na ilikuwa ya maudhi dhidi ya Rais na ililenga kuchochea wananchi kuipinga na kuichukia Serikali.

Akizungumza mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwampamba, shahidi huyo aliongeza kuwa kauli hiyo ya Lissu pia ililenga katika kuhatarisha usalama wa taifa kama ingesambazwa sehemu kubwa.

Naye Wakili wa Lissu, Peter Kibatala alimtaka shahidi huyo kuieleza mahakama ni nani ambaye mteja wake alikuwa anamtaja kama ‘dikteta uchwara’ na taifa analolizungumzia kwenye madai yake.

Akijibu maswali ya Wakili Kibatala, ASP Kimweli alisema kuwa hakufahamu kiuhalisia ni nani ambaye Mbunge huyo alikuwa akimrejea katika matamko yake na pia hakufahamu ni taifa gani alilokuwa akilimaanisha.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Januari 18 mwakani itakaposikilizwa tena mahakamani hapo. Lissu yuko nje kwa dhamana.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx