Baada ya mashabiki kuwapigia kura mshindi wa mfurulizo Yaya Toure amepigwa chini.
Mshambuliaji wa pembeni wa klabu ya Leicester City Riyad Mahrez ametangazwa kua ni mchezaji bora wa BBC Afrika.
Riyal mwenye asili ya Algeria, msimu uliopita alishinda kombe la ligi kuu ya nchini Uingereza akiwa na klabu ya Leicester City ambapo alionesha uwezo mkubwa na jitihada zaidi na kwasasa timu yao ya Leicester City imeingia katika hatua ya 16 bora ya ligi ya mabingwa ya Ulaya ( UEFA)
Mahrez alifanikiwa kufunga magoli 17, na kutoa pasi za mwisho 11 katika ushindi wa kombe la ligi msimu uliopita na ushiriki wa ligi ya mabingwa ni vigezo vilivyomuwezesha kushinda tuzo hii.
Mahrez mwenye umri wa miaka 25 alipigiwa kura na mashabiki kutoka sehemu mbali mbali za dunia, mwishowe akaibuka mshindi kati ya wachezaji bora wa Afrika; alioshindana nao ni Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Sadio Mane na Yaya Toure.
Mahrez amesema mbele ya BBC baada ya kupokea tuzo " Ni kitu kikubwa kwa wachezaji wa Afrika, kwa mimi najisikia furaha na pia najivunia"
"Pia napenda kuwashukuru mashabiki wangu wote wa Algeria kwa hii tuzo na pia kwa kwa familia yangu. Natakiwa kuendelea mbele na kujituma zaidi katika mpira na kuangalia kipi nitakifanya"