MWANDISHI: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA
Nikamvuta
na kumuingiza chooni, mikamuonyesha bomu lilipo, Sote tukajikuta
tunashangaa kutokana bomu hilo limebakisha sekunde hamsini na tisa,
kabla halijalipuka na sote hapa hatujui jinsi ya kulitegua, na muhudumu
akaanza kulia, akijaribu kunikumbatia kwani mwisho wetu umefika.
"Una chochote cha kukatia"
Nilizungumza
huku nikimtoa muhudumu huyu, mwilini mwangu, kwani kukumbatiana kwetu
sio suhulisho la bomu hili kuacha kuacha kulipuka. Hakunijibu zaidi ya
kubabaika, kwa mawenge yaliyo mchanganya kupita maelezo. Akaanza
kujipapasa huku mwili mzima ukimtetemeka kwa woga, akatoa, kikatia
kucha(Nail cutter), akaitupa chini huku akiendelea kuikagua mifuko ya
nguo zake alizo zivaa. Kwa haraka nikaokota kikatia kucha, nikapiga
magoti chini, huku nikiwa ninajiamini kwa lile ninalo kwenda kulifanya.
Sekunde za bomu hili, zikazidi kurudi nyuma, huku zikiwa zimebakia
sekunde thelathini na mbili kabla halijalipuka. Nikaanza kuzichambua
nyaya nyingi ndogondogo zipatazo ushirini, zikiwa na rangi tofauti
tofauti.
"Ishirini na tano"
Muhudumu aliniambia, huku macho yake akiwa ameyatumbulia kwenye bomu, linalo zionyesha sekunde hizo, zinavyo rudi nyuma.
"Mungu wangu"
Nilizungumza huku nikizidi kuchanganyikiwa, kwani sikujua ni waya upi unanipasa kuukata, ili kulizuia bomu hili kuto kulipuka.
"Kumi na tano"
Nikashika nyaya moja nyekundu na kuikata, chakushangaza, bomu likaendelea kurudisha sekunde zake nyuma.
"Nane"
Nikazidi kuchanganyikiwa, na kukata wanya mweusi, hali ikawa ni ile ile.
"Tano"
Mikono
yote, ikazidi kutetemeka hadi nikaangusha kikatia kucha, nikakiokota
kwa haraka, hata kukaa mkononi vizuri, nkawa ninashindwa kukishika.
"Tatu"
Nikamuona
muhudumu, akipiga ishara ya msalaba akiashiria mwisho wetu ndio
unakaribia, nikashika waya wa rangi ya kijani, sekunde ikawa imebaki
moja, nami nikawa nimeukata. Sekunde hiyo ikasimama hapo hapo na bomu
kuzima. Nikashusha pumzi nyingi, huku mwili wangu wote ukiwa umesha vuja
jasho lakutosha hadi shati nililo livaa, likawa limelowana kabisa.
Kumtazama muhudumu nikamkuta akiwa ameyafumba macho yake huku jasho
likimwagika shingoni nwake.
"Tumefanikiwa"
Nilizungumza
kwa sauti ya unyonge huku nikimtazama usoni muhudumu, akayafumbua macho
yake taratibu, huku akihema. Akalitazama bomu nililo lichomoa na
kulishika, akabaki akiwa ameduwaa. Akanishika mkono taratibu na
kuninyanyua, akanikumbatia huku akilia kwa furaha.
"Asante Mungu, kweli wewe ni mwema. Hakuna kama wewe"
Alizungumza
huku akiendelea kulia, nakunifanya na mimi machozi kunimwagika kwani
sikutarajia kama nitaweza kufanikiwa kulitegua bomu hili, taratibu
akaniachia, huku akijifuta machozi usoni
"Unaitwa nani?"
"Eddy, Eddy Godwin"
"Am Tasiana, from Arusha Tanzania"(Mimi ni Tasiana natokea Arusha Tanzania)
"Mimi pia natokea Tanzania, ila A leve nilisoma Arusha"
"Waooo, nashukuru kukufahamu"
Tasiana
akanikumbatia kwa mara ya pili, akawasiliana na marubani wa ndege hii,
kupitia kijisimu kidogo wanacho kitumia kuwasiliana, wakamuomba tuelekee
kwenye chumba walipo, tukiwa na bomu hilo, ila tuhakikishe hakuna
abiria atakaye liona, ili kuto hatarisha amani ya walio wengi.
Tasiana
akachukua mfuko mtupu, mweusi. Akaliweka bomu, nikaongozana naye hadi
chumba cha marubani. Tukawaelezea hali halisi juu ya tukio zima na jinsi
mchungaji Frank, alivyo nipa vitisho nikiwa ninapishana naye kwenye
mlango wa chooni.
"Hakuna
aliye toka ndani ya ndege, ngoja tukifika Afrika kusini, tutafanya
upelelezi kabla watu hawaja ruhusiwa kushuka kwenye ndege"
Rubani mmoja alizungumza huku akilitazama tazama bomu hilo nililo mpatia.
"Ukimuona si utamkumbuka?"
"Ndio, nilikuwa nimekaa naye ila simuoni kwenye siti yetu"
"Ulikaa siti gani?"
Nikamtajia
rubani, huyo herufi ya siti niliyo kuwa nimekaa, akatazama mkanda
mzima, kwenye kiji tv chao kidogo unao rekodiwa na kamera zilizo tegwa
kila kona ya ndege. Tukamuona mzee huyo akiingia kwenye moja ya chumba
walicho dai ni stoo, chenye gazi za kushukia chini, kunapo hifadhiwa
mizigo mikubwa mikubwa.
"Ngoja nimfwate"
Nilizungunza kwa kujiamini, huku nikiwatazama marubani hawa wapatao wanne, huku wawili wakiwa niwasaidizi.
"Itaweza kumkamata?"
"Nitahakiksha nalifanikisha hilo"
Wakanitazama machoni, mkuu wao akanipa ruhusa.
"Tuongozane"
Tasiana aliomba tuongozane pamoja.
"Wewe baki, ngoja nikajaribu kulifanya na hili kama nitafanikiwa"
"Tafadhali twende pamoja"
Tasiana
aling'ang'ania kwenda, ikanibidi nimkubalie tu. Tukaongozana hadi
kwenye chumba hicho, pasipo wasafiri wezangu kuelewa kitu gani kinacho
endelea, hakikuwa chumba kikubwa sana, kwani kina ngazi zakushuka chini
kulipo na mizigo mikubwa. Tukafanikiwa kushuka chini, kwa wingi wa
mizigo iliyo fungwa kwenye mifurushi mikubwa, ilitufanya tubaki tukiwa
tumesimana na kuduwaa.
"Atakuwa wapi?"
Tasiana aliniuliza kwa sauti ya chini, huku tukiendea kupepesa pepesa macho yetu kila kona ya eneo hili lilolo kubwa.
"Nifwate nyuma na kuwa mkimya"
Tukaanza
kupita kwenye vinjia, vilivyo tenganishwa kwa maburungutu makubwa ya
mizigo. Nikaanza kupata wasiwasi, baada ya kukuta shati alilo kua
amelivaa mzee yule, likiwa chini. Tasiana akataka kuliokota ila
nikamzuia asifanye hivyo.
"Kwa nini nisiliokote?"
Nikatingisha
kichwa nikimuashiria Tasiana asifanye chochote dhidi ya shati
hilo.Tukalipita, hatua kumi mbele, tukakuta suruali aliyo kuwa ameivaa.
Kwa kutumia mguu nikaisogeza kuitazama kama kuna kitu kimefunikwa, ila hatukuona kitu.
Arufu
ya moshi wa sigara, ukaanza kuingia kwenye pua zetu, ulitokea upande wa
pili wa sehemu ilipo mizigo hiyo. Tukapiga hatua za tahadhari hadi
sehemu inapo tokea harufu ya moshi huo wa sigara, tukakuta kipande cha
sigara kikiwa chini, kikiendelea kuteketea taratibu.