Kanali Ngemela Lubinga (katikati), kulia ni Msaidizi wa Kanali Lubinga, Meja Joseph Masanja na kushoto ni Kapteni Swaleh Omar.
****
Wakati
watu mbalimbali wakiwa na maoni tofauti kuhusu Chama cha Mapinduzi
(CCM) kupitia Halmashauri Kuu yake kumteua Kanali wa Jeshi la Wananchi
wa Tanzaia (JWTZ) kuwa Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Siasa na
Uhusiano wa Kimataifa, mwenyewe ameibuka na kutolea ufafanuzi uteuzi
huo.
Kanali
Ngemela Eslom Lubinga amesema kuwa alishastaafu utumishi wake jeshini
na kuwa angeweza kutumikia chama cha siasa kwani si mtumishi wa jeshi
hilo tena. Kanali Lubinga aliyekuwa Msemaji wa JWTZ alisema kuwa
alistaafu utumishi katika jeshi kuanzia Disemba 2 mwaka huu. Aidha,
alisisitiza kuwa alijiunga na Chama cha Mapinduzi mwaka 1979.
Kikubwa
kilichozua maswali kuhusu uteuzi huu ni kwa sababu wanajeshi na
watumishi wengine wa umma hawaruhusiwi kuwa wanachama wa vyama vya
siasa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waraka wa Utumishi
wa mwaka 2015 unakataza watumishi wa umma kuwa wanachama wa vyama vya
siasa lakini unatambua haki yao ya msingi ya kupiga kura.
Badhi
ya maswali yaliyoulizwa na watumiaji wa mitandao ya kijamii ni lini
Kanali Lubinga alijiunga na CCM kiasi cha kuweza kuteuliwa katika nafasi
ya juu kiasi hicho? Kama alijiunga na chama mwaka 1979 inaonyesha wazi
kuwa alikiuka katiba ya nchi inayowataka wanajeshi kutojiunga na vyama
vya siasa.
Akijibu
swali hilo Kanali Lubinga alisema kuwa wakati wa mfumo wa chama kimoja
wanajeshi waliruhusiwa kujiunga na chama cha siasa na kuwa baada ya
kuanza mfumo wa vyama vingi mwaka 1992 ndipo walizuiwa na kadi
walizokuwa nazo zilichukuliwa.
Kanali
Lubinga aliendelea kusema kuwa kadi zile hazikutupwa bali zilihifadhiwa
na hivyo baada ya kustaafu Disemba 2 mwaka huu akachukua kadi yake na
kuendelea na uanachama wake.
Wengi
waliokosoa uteuzi huo walitaka kuhakikisha kuwa siasa za nchi
haziathiri utendaji wa majeshi yetu na utumishi wa watumishi wengine wa
umma.