Mke
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli jana
Jumapili ameungana na Wakristo wenzake wa Kanisa Katoliki Parokia ya
Mtakatifu Petro iliyopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam ikiwa ni wiki
kadhaa tangu alipougua na kulazwa hospitali.
Akiwa
mwenye afya njema na furaha Mama Magufuli aliyekuwa pamoja na Mke wa
Waziri Mkuu Mama Mary Majaliwa walisali ibada ya asubuhi katika kanisa
hilo na baadaye kusalimiana na waumini nje ya kanisa.
Baada
ya kumalizika kwa Ibada, baadhi ya Waumini wa Kanisa hilo walielezea
furaha yao ya kumuona Muumini mwenzao akiungana nao katika ibada na
walimuombea afya njema.
“Nimejisikia
furaha sana kumuona Mama Magufuli amekuja Kanisani akiwa na afya njema
na uso wa bashasha, na ninamuombea kwa Mungu aendelee kumsimamia” alisema Mama Mabula.
“Nimeshukuru
sana kumuona Mama yangu Mama Magufuli, Mwanajumuiya mwenzangu
Kanisani, huku afya yake ikiwa imetengemaa zaidi, tunamshukuru sana
Mwenyezi Mungu na tunamuombea aendelee kumpigania afya yake izidi kuwa
imara” alisema Thomas Simon.
Mwezi
uliopita Mama Janeth Magufuli aliugua na kulazwa katika wodi ya
Sewahaji iliyopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambako alipata
matibabu kwa siku mbili na kisha kuruhusiwa.