![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEijwQd8QbgmKBiP87Oq_JpZTD6y2q0MHMUav_jqIPOWVc5EsTelUFmkEkZK_9xFpsFLLrCkrQhIahds_n5XK0Wgdp6FmXx-NxN3JgwWGLTMGf6VJAIWFA5giaCx57wj2cRvrIwbq6_AZ_o/s640/NAPE+SALAMA+%25282%2529.jpg)
Waziri Habari,
Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye amesema amesikia kilio cha
wasanii kuhusu kuwabana katika kazi zao hususan kwenye video za muziki
na kuahidi kufumba jicho moja ili kuwapa uhuru kiasi.Waziri Habari,
Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye akiwa na Salama Jabir katika
Tuzo za EATV
(Picha na Othman Michuzi)
Ametoa ahadi hiyo wakati
akizungumza kwenye tuzo za EATV zilizotolewa kwa mara ya kwanza
Jumamosi hii kwenye ukumbi wa Mlimani City.
“Tutaachia kidogo
hatutabana sana," alisema Nape. “Na mimi nimepita mtaani naambiwa ‘Nape
mmebana sana.’ Wakati mwingine tunataka kufanya mambo tunaambiwa
tumepitiliza. Wakati mwingine tutafumba jicho moja watu wapitilize
kidogo ili mambo yaende sawa sawa,” alisisitiza waziri huyo aliyekuwa
mgeni rasmi kwenye tuzo hizo.
Kwa muda mrefu Baraza la
Sanaa la Taifa, BASATA lililo chini ya wizara yake, limekuwa
likilaumiwa kwa kutoa adhabu kali kwa wasanii kwa kile inachosema ni
kuvunja maadili.