![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEjJtme2FhnXwj62zMJHy3zmQUTuvnuUvdvy555mMhhYDEtX2FTNzMyPXd1rMF04hxRieTXdjrG9vSn8p0YBwZ-hgIVV5Vjs6LQvuASTGDCS9bNcziPfUc5gUQUTm57H9fJvVpI2syPXUp4/s640/SAMIA-SULUHU.jpg)
“Tumeshuhudia kukimbiwa
na wawekezaji kadhaa kwa sababu mwekezaji anakuja anataka kuwekeza
Tanzania, miaka mitatu hajapata jawabu kama ndio wekeza au toka nenda
zako, anazungushwa anapigwa taasisi moja kwenda nyingine, hili lifike
mwisho,” alisema.
Samia alisema serikali
itakuwa makini sana kusimamia suala hilo kwa nguvu, kutokana na kwamba
kumekuwa na upotevu mkubwa wa uwezeshaji katika uchumi wa nchi.
Alitaja pia kuwa tatizo
la rushwa kuwa moja ya sababu inayowakimbiza baadhi ya wawekezaji wenye
nia ya kuja kuwekeza nchini na kwamba wekezaji wanaotajwa kukimbia
kuwekeza nchini wengi wao ni wanaogoma kutoa rushwa ili kupata majibu ya
kama wanaruhusiwa au hawaruhusiwi kuwekeza na hufanya hivyo
wanapotakiwa kuhonga.
Samia alisema azma ya
serikali ya kufikia uchumi wa viwanda mwaka 2025 kwa kutumia rasilimali
za ndani itawezekana kama watumishi waliokabidhiwa dhamana ya kukusanya
mapato na kusimamia matumizi ya fedha za Serikali watazingatia maadili
ya utendaji kazi na kuweka mbele maslahi ya umma.
“Viongozi wa Umma
wasimamie vema watumishi walio chini yao, kuna mtindo katika baadhi ya
ofisi za Serikali kufanya kazi zao bila kufuata taratibu zilizoainishwa
kwenye mikataba ya huduma kwa wateja…hili ni tatizo kubwa ndani ya
Serikali yetu,” alisema.