test

Jumamosi, 12 Novemba 2016

Tundu Lissu Alikumbuka Bunge la Mh. Sitta



Wabunge mbali mbali wa vyama vya upinzani Bungeni, wametoa yale yanayosemwa ya moyoni juu ya mwenendo wa Bunge kwa sasa, wakifananisha na ule ambao marehemu Samuel Sitta alikuwa akiuendesha.

Mbunge wa Singida Mashariki, Mh. Tundu Antiphas Lissu
Wakitoa salamu za rambi rambi kwa familia, wabunge na waombolezaji waliokuwa Bungeni mjini Dodoma wakiaga mwili wa aliyekuwa Spika wa Bunge la 9 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samuel John Sitta, wabunge kutoka vyama mbali mbali wamemuelezea marehemu kama mtu aliyesimamia haki katika Bunge, bila kujali itikadi za vyama na kiongozi mwenye mfano wa kuigwa na wengine, huku wengi wakiguswa na salamu zilizotolewa na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Antiphas Lissu.

Tundu Lissu ambaye pia alitoa salamu hizo kwa niaba ya CHADEMA, alisema Mh. Sitta alitaka Bunge lenye meno, lenye uwezo wa kufanya maamuzi ya nchi kama mhimili wa nchi, na sio kuwa kivuli cha serikali.

"Kwa muda mrefu Bunge liliishi katika kivuli cha serikali, Samuel Sitta aliliondoa Bunge kutoka katika kivuli hicho, alitaka Bunge lenye meno, alitaka Bunge linaloisimamia na kuidhibiti serikali, alitaka kama mhimili wa dola na sio msindikizaji wa dola, ndio zawadi kubwa ya utumishi wake mrefu kwa Tanzania", alisema Tundu Lissu. 

Tundu Lissu alihitimisha kwa kutaka watanzania na wabunge wenzake kumuenzi marehemu Samuel Sitta kwa kusimamia yale aliyoyapigania, katika kipindi cha uhai wake.

"Namna bora ya kumkumbuka ni kujiuliza hili ni Bunge ambalo alilitaka liwe!? ambalo angetaka kuliongoza? Tukijiuliza hilo na tukayatafutia majibu yake, tutakuwa tumemkumbuka kwa namna ambayo anastahili", alisema Tundu Lissu.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx