Skip to content
Freeman Mbowe ni mbunge wa jimbo la Hai na mwenyekiti wa CHADEMA taifa
ambaye leo November 11 2016 alipata nafasi ya kuongea wakati wa kuuaga
mwili wa Spika mstaafu Samuel Sitta ndani ya bunge Dodoma.
‘Mzee Sitta tulimuona kama kiongozi asiekua mbaguzi wa kiitikadi,
aliamini katika kubadilisha kwenda kwenye ubora katika nafasi yote ya
utumishi wa UMMA aliyoihudumia, alikua mtu aliejaza matumaini watu wote
aliowaongoza wakati wote, alikua mtu wa kuunganisha makundi yote‘ –
Mbowe
‘Mara nyingine sisi wapinzani tulipata wakati mgumu sana wa kumtambua
Mheshimiwa Sitta bado ni kada wa CCM sababu alikua na uwezo wa kutujaza
matumaini, kutupa fursa ya kutusikiliza lakini mwishoni tunakuja
kugundua bado ni wa CCM‘ – Freeman Mbowe
Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi
xxxxxxxxxxxxx