Kauli hiyo, “umekula maharage ya wapi” ilipata umaarufu Machi mwaka jana baada ya kutolewa na Askofu Gwajima wa Kanisa la Ufufuo na Uzima na baadaye kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikidaiwa kumlenga Askofu Mkuu wa Jimbo la Dar es Salaam, Muadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Kama ilivyotokea kwa Gwajima kushtakiwa kwa tuhuma za kutoa kauli hiyo na nyingine zilizosambaa mitandaoni, Mbunge huyo alijikuta akiitumia kauli hiyo kumuuliza Spika Ndugai wakati wa kikao cha Bunge na kuishia kupewa onyo kali.