Serikali
ya Mapinduzi Zanzibar inapenda kukanusha taarifa kutoka Kwenye baadhi
ya Mitandao ya Kijamii ikidai kwamba, Mhe. Kamishna wa Tume ya Uchaguzi
Zanzibar, Balozi Omar Ramadhan Mapuri (pichani) amefariki dunia.
Taarifa
Rasmi ya Serikali ni kwamba taarifa hizo ni za uongo na hazina hata
Chembe ya ukweli. Mhe. Kamishna Balozi Mapuri yupo hai na afya yake iko
vizuri.
Mheshimiwa
Balozi Omar Ramadhan Mapuri ambae kwa sasa ni Kamishna wa Tume ya
Uchaguzi Zanzibar alilazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili
alikokuwa akipata matibabu na baada ya kupata huduma kutoka kwa
madaktari, Mheshimiwa Balozi Mapuri aliruhusiwa kurejea nyumbani siku ya
Jumamosi Novemba 12 baada ya afya yake kuimarika.
Serikali
imesikitishwa na taarifa za uvumi na uzushi uliosambazwa jana na leo
kwenye mitandao ya kijamii, taarifa hizi sio za kweli na tunawaomba
wananchi wazipuuze.
Aidha,
Serikali inapenda kuvionya vyombo vya habari na Mitandao ya kijamii
kuacha kusambaza taarifa za uongo kuhusu viongozi wa Serikali.
Imetolewa na :
Dk. Juma Mohammed Salum
Kny Mkurugenzi
Idara ya Habari MAELEZO
Zanzibar