ILIPOISHIA
Majibu
ya mlinzi huyo mwenye roho ya kikatili sana, yakaustua moyo wa makamu
wa raisi kwani ameamini kwamba taarifa hiyo si nzuri kwa upande wake.
“WHAT………!!!”
Makamu
wa raisi alijikuta akiishiwa na nguvu, akajibwaga kwenye sofa lililopo
karibu yake akibaki amemtumbulia mimacho mlinzi wake huyo.
ENDELEA
Makamu wa raisi akakaa kimya kwa muda akifikiria ni kitu gani anaweza kukifanya, gafla akasimama huku akitabasamu
“Bimgo”
Alizungumza
huku akimuomba mlizi wake simu. Akaminya baadhi ya namba kisha
akaiweka simu yake sikioni, baada ya dakika kadhaa ikapokelewa na sauti
nzito ya kiume.
“Yaa ni mimi”
Makamu wa raisi alizungumza, na kumfanya mtu aliye ipokea simu hiyo kuweza kujua anazungumza na nani.
“Kuna mgonjwa hapo hospitalini kwako, somebody Samsoni. Ninahitajia umuondoe kwenye ramani ya dunia”
“Sawa nimekuelewa muheshimiwa, uishi daiama”
“Asante”
Makamu
wa raisi akakata simu huku akiwa katika tabasamu pana. Ulinzi kwenye
hii hoteli yake aliyo ijenga kwa usiri mkubwa pasipo serikali ya
Tanzania kuweza kuifahamu, uliendelea kuimarika kila kona huku vijana
wake wanao muunga mkono wakiwa makini sana kuhakikisha kwamba hakuna mtu
anaye weza kufahamu kwamba kiongozi huyo anaye tafutwa na serikali ya
Tanzania yupo kwenye hoteli hii kubwa ya kitalii.
***
Tayari
mawasiliano yalisha fanywa kwenye hospitali ya Muhimbili, ili chumba
alicho lazwa Samson kifanyiwe ulinzi wa hali ya juu. Askari wenye
bunduki nzito walisha weka ulinzi eneo zima la hospitali wakihakikisha
kwamba anapofika Raisi Praygod Makuya, kila jambo linakuwa kwenye mstari
na hakuna tatizo la kijinga litakalo kwenda kujitokeza.
Hali
ya Samson, kidogo inaleta matumaini kwa madaktari, hii ni baada ya
kutolewa risasi mwlinini mwake, ambazo kwa bahati nzuri hazikuweza
kuleta madhara makubwa sana kwenye mwili wake.
“Nahitaji kumcheki mgonjwa”
Daktari
mkuu wa kitengo cha upasuaji aliwaambia askari wawili walio simamam
mlangoni mwa chumba alichopo Samson. Mmoja wa askari akachukua
kitambulisho kinacho ning’inia kwenye kifua cha daktari huyo na kulisoma
jina lake, ili kudhibitisha kwamba kweli ni daktari wa hospitali hiyo,
alipo jiridhisha akamruhusu daktari huyo kuingia ndani ya chumba hicho.
Dokta Maliki, akasimama pembeni ya kitanda alicho lalala Samson, anaye hemea kwa mashine maalumu za kupumulia.
“Nilazima umfe mwanaharamu wewe”
Dokta
Maliki alizungumza huku akivaa gloves zake nyeupe kwenye viganja vyake,
ili kutoweza kuacha alama za vidole pale atakapo fanya mauaji yale alio
agizwa na Makamu wa raisi. Alipo hakikisha gloves zake zipo vizuri,
akachomoa mashine iliyo wekwa kwenye kinywa cha Samson, akasababisha
Samson kuanza kujitingisha tingisha taratibu, akijaribu kuipigania roho
yake na umauti kwani hewa iliyokuwa inaingia kwenye mapafu yake
imekatishwa.
***
“Endesheni haraka”
Rahab
alizungumza huku akihangaika hangaika kwenye siti aliyo kalia hadi
Raisi Praygod akamshangaa kwani ni kama mtu anaye hitaji kuweza kuliwahi
jambo fulani.
“Kwani vipi mke wangu?”
“Kuna tatizo fanyeni haraka”
“Wapi…!!?”
“Dereva ongeza kasi tafadhali”
“Madam sote tunakwenda kwenye mwendo mmoja nikiongeza kasi mimi naweza kusababisha ajali”
Dereva
anaye waendesha alizungumza kwa ukanini wa hali ya juu kwani ndivyo
sheria ya kazi yake inavyo zingatia, kwenye msafara kama huo wote huwa
wanaendesha katika mwendo kasi unao fanana.
“Lakini tunakaribia kufika mke wangu”
Raisi
Praygod alimtoa wasiwasi Rahab, aliye yafumba macho yake kwa haraka,
kama mtu anaye jaribu kuvuta hisia ya jambo fulani. Kila alipo jaribu
kuvuta hisia dhidi ya jambo linalo kwenda kumtokea Samson, akashindwa
kuona ni nini kinacho kwenda kutokea.
“Pleaseeeee”
Rahab
alizungumza kwa sauti ya juu huku akizidi kuyafumba macho yake kwa
nguvu, hadi damu za puani zikaanza kumchuruzika taratibu, Raisi Praygod
akajaribu kumshika mkono mke wake kutazama ni nini kinacho msumbua, ila
akajikuta mkono wake ukisogezwa kwa nguvu na mke wake huyo hadi akabaki
ameduwaa.
Rahab,
akashuhudia jinsi shingo ya Samson inavyo kandamizwa kwa nguvu na mtu
aliye valia mavazi meupe, baada ya muda kidogo Samson akatulia kimya,
ikiashiria tayari amesha yapoteza maisha yake. Rahab akayafumbua macho
yake huku akishusha pumzi taratibu, machozi ya uchungu yakaanza
kumwagika usoni mwake.
“Mke wangu unatatizo gani?”
Raisi
Praygod aliuliza huku akiwa na wasiwasi mkubwa, Rahab akatingisha
kichwa akidai hakuna tatizo ambalo limejitokeza. Rahab akajifuta damu
zilizo kuwa zikimwagika, huku akiamini kwamba safari wanayo iendea haina
umuhimu tena kwao. Kwani mtu wanaye mfwata tayaria amesha uawa kinyama,
na mtu amabaye hakuiona sura yake.
***
Dokta
Maliki, alipo hakikisha kwamba tayari amesha muua Samson kwa kuiminya
shingo yake, akarudishia kila kitu alicho kitoa kwenye mwili wa Samson,
ikiwemo mashine inayo msaidia kuhema. Baada ya mashine hiyo kurudishiwa
kwenye mdomo wa Samson, ikaaonyesha mstari mwekundu ulio nyooka,
ukiashiria kwamba mtu huyo tayari amesha poteza maisha. Dokta Maliki
akatoka ndani ya chumba hicho.
“Hakikisheni hakuna anaye ingia humu ndani, mgonjwa anahitaji kupumizika”
Aliwaambia
askari hao ambao hakuna aliye kuwa akifahamu ni kitu gani kinacho
endelea, Dokta Maliki akaanza kutembea kwenye kordo ndefu kuelekea nje,
na muda huu hakuhitaji kukaa tena hospitalini kwani tayari anatambua ni
kitu gani alicho kifanya na endapo atajulikana kama yeye ni muuaji, basi
adhabu kali itaambatana naye.
Akiwa
katika eneo la maegesho ya magari, gari kadhaa zinazo ashiria zimembeba
kiongozi mkubwa zikasimama, ikamlazimu kuangalia ni kiongozi gani
ambaye anashuka. Mlango wa gari moja ukafunguliwa akashuka binti mmoja
pamoja na jaama ambaye ni mara yake ya kwanza kuiona sura yake
“Huyu ni nani?”
Alijuliza,
huku akiendelea kumtazama jamaa huyo anaye wekewa ulinzi mkubwa kama
kiongozi wa nchi. Macho ya dokta Maliki yakagongana na macho ya Rahab,
aliye mtazama kwa muda huku akionekana kama msichana huyo anamtambua
Dokta Maliki. Raisi Praygod baada ya kumuona mke wake anamshanga sana
dkatari aliye simama kwenye moja ya gari huku akiwa na funguo mkononi,
ikambidi amshike mke wake mkono.
“Baby twende ndani”
Rahab
akaondoka na Raisi Praygod ambaye sura yake halisi imefunikwa na sura
bandia ambayo hakuitaji sura yake iweze kuonekana na mtu wa iana yoyote
zaidi ya walinzi wake wanao fahamu kwamba ni yeye. Dokta Maliki akiingia
ndani ya gari lake na kuondoka katika eneo la hospitali ya Muhimbili
huku moyoni mwake akiwa na furaha ya kuweza kukeleza kazi ya kiongozi
wake anaye mtumikia.
Raisi Praygod moja kwa moja akapelekwa kwenye chumba alicho lazwa
Samson, huku akiwa na mke wake pamoja na daktari mkuu wa zamu, aliye
weza kuitambua sauti ya raisi Praygod.
“Samahani dokta. Dokta Maliki ameagiza asiingie mtu ndani ya chumba hichi”
Askari
walio achiwa jukumu la kulinda katika chumba hicho waliwazuia Raisi
Praygod, Rahab pamoja na daktari huyo wa zamu pasipo kufahamu kwamba
huyo wanaye mzuia ndio raisi wao
***
Baada ya hali kutulia, kwenye hoteli alkliyo fikizia waziri wa mambo ya
nje ya Marekani, mkuu wa askari nchini Russia akiwa ameongozana na
vijana wake wawili, wakaelekea sehemu walipo fichwa viongozi hao wawili.
Kila mmoja akashikwa na butwaa baada ya kukuta miilii ya walinzi wote
ikiwa imezagaa chini huku ni raisi wao akiwa amekaaa kwenye sakhafu huku
akiendelea kuugulia maumivu makli ya jeraha la risasi aliyo pigwa.
Kwa
haraka wakafanya mawasiliano na askari wengine wa markani waliopo nje
ya hoteli hiyo wakiendeleza ulinzi. Kuhakikisha kiongozi wao anaye
lindwa ndani hapatwi na tatizo lolote. Kitendo cha kukuta kiongozi wao
ameua, kila mmlinzi akajikuta akichanganyikiwa, kwani hakuna aliye elewa
tukio hilo limefanywa na nani, huku walinzi wote wakuaminika wakiwa
wameuwa kikatili.
Wakafanya
mawasiliano haraka moja kwa moja kwenye ikulu ya Marekani na kutoa
taarifa hiyo iliyo wachanganya kuanzia raisi pamoja na jopo lake zima la
ulinzi. Uchunguzi wa kina ukaanza kufanyika kwa kina, huku kamera za
eneo hilo zikichunguzwa kujaribu kumuona nani ameusika na mauaji hayo.
Cha kushangaza kamera zote za eneo lililo tokea maauji, hazikuweza
kuonyesha tukio hilo, hapo ndipo wakagundua kuna mchezo ambao
umefanyika.
(muda mchache kabla ya tukio)
Baada
ya Agnes, kushindwa kumuua waziri wa mambo ya nje wa Marekana, akiwa
mbali kwenye sehemu walipo jificha, akili ya Anna ikatambua moja kwa
moja ikatambua kwamba ni lazima Agnes atashuka na kwenda kutekeleza
tukio hilo kwenye hoteli hiyo. Kifaa maalimu kilicho ingizwa mwilini mwa
Agnes, kiliweza kumuonyesha kila sehemu anayo kwenda.
Anna akaomba kupewa kazi moja ya kumlinda rafika yake huyo ambaye anaiendea kazi moja ya hatari sana.
“Utamsaidiaje?”
Bwana
Rusev alizungumza huku akimtazama Anna machoni. Anna akamuomba
muendesha mitambo katika chumba hicho walichopo aweze kumpisha kwenye
kiti kwani kuna kazi anahitaji kuweza kuifanya. Kwa utaalamu alio kuwa
nao Anna, akaanza kucheza na kamera za ulinzi zilizopo kwenye eneo hilo
kwa kutumia computer iliyo unganishwa mitambo ya Satelaite, alicho anza
kukifanya ni kutafuta namba za siri ambazo zinaongoza kamera zote
zilizopo kwenye eneo hilo, kwa bahati nzuri akafanikiwa kuzipata, alicho
kifanya ni kuweza kugandisha kila kamera anapo pita Agnes, jambo ambalo
halikuweza kustukiwa na wataalamu walipo kwenye chumba maalumu kwenye
hoteli hiyo katika kuongoza kameza zaidi ya alfu moja zilizopo katika
eneo zima la hoteli.
Tukio
la Agnes kumteka kijana mwenye mavazi ya zima moto halikuweza kunaswa
na kamera za hoteli, zaidi ya wataalamu hao kunao kila eneo lipo salama
kupitia tv zao nyingi zilizomo ndani ya chumba hicho.
Agnes
anaingia kwenye eneo walilopo viongozi, camera zote ziliweza
kugandishwa na Anna, zikawa zinaonyesha uneo hilo likiwa limetulia,
kumbe walinzi wanao walinda viongozi wao wapo kwenye wakati mgumu,
wakiadamishwa na binti mmoja ila mwenye uwezo mkubwa kupita maelezo.
Hadi
Agnes anatoka katika eneo hilo hapakuwa na camera iliyo weza kumnasa
sura yake, na hapakuwa na mtu aliye weza kustukila swahala hilo. Watu
waliomo ndani ya chumba hicho wakajikuta wakipiga makofi kwani kwa kazi
waliyo ifanya mabinti hao, ni kazi kubwa sana yakutumia akili pasipo
nguvu nyinngi.
***
Mahojiano ya haraka yakafanywa kwa Raisi wa Russia aweze kueleezea
muuaji huyo wa kike anaonekana vipi. Huku akiendelea kufanyiwa matibabu
na madaktari bingwa. Raisi akaendlea kutoa maelezo jinsi binti huyo
anayo onekana. Wataalamu wa kuchora waziadi kuendela kuichora sara ya
binti huyo hadi ikakamilika na kupata sura halisi ya Agnes. Picha hiyo
kwa haraka ikatuma makao makuu ya ujasusi nchini Marekani Washinton DC.
Sura hiyo ikaningizwa kwenye mitambo maalumu ambapo, kwa kutimia
satalaite wakaanza kuitafuta ni wapi sura hiyo inapaikana.
“BINGOOOO”
Mtaalamu
mmoja alizungumza baada ya kumpata msichana huyo ambaye bado anaonekana
hajatoka kwenye nchi ya Rusia. Kila kona ya mipika picha ya Agnes
ikasambazwa kwa haraka kwa kila askari, vituo vyote vya mabasi, reli,
anga pamoja na bandari. Vikaimarishwa ulinzi mkali, huku askari wa
kutosha kutoka Marekani, wakihakikisha wanamtia nguvuni binti huyo anaye
onekana ni gaidi wa kimataifa.
Agnes
pasipo kufahamu chochote kinacho endelea, akiamini kwamba kila kitu
kipo sawa, akafika kwenye kituo cha treni. Akiwa katika moja ya dirisha
la kukatia tiketi za treni, wanajeshi wawili wa kimarekani, wakiwa na
mbwa wakasimama mbele yake huku wakimkazia macho, huku mmoja wao
akijaribu kuchomoa bastola yake kwa ajili ya kumdhibiti Agnes kwani
tayari wamesha mtambua yeye ndio muuaji wa kiongozi wao bwana Paul Henry
Jr.
SHE IS MY WIFE(46)
Gafla,
wanajeshi hao wawili walio simama, mbele ya Agnes, wakaanguka chini
huku wakitoa milio mikali ya maumivu, mbwa walio washika wakatoa milio
mmoja na kuanguka nao chini. Hata Agnes mwenyewe akabaki ameduwaa kwania
hakujua ni nani aliye weza kulifanya tukio hilo la kuwaangamiza
wanajeshi hao walio anza kuvuja damu kwenye miili yao.
Wananchi
walipo karibu wakaanza kupiga makelele huklu wakikimbia kimbia.
Makelele hayo yakawafanya askari pamoja na wanajeshi wengine kwenye eneo
hilo kukimbilia katika sehemu kelele hizo zinatokea. Agnes akataka
kujijichanganaya na wananchi hao, gafla akadakwa mkono wake kwa nyuma,
akageuka kwa haraka huku akiwa emerusha ngumi iliyo pita hewani baada ya
mtu huyo kuweza kuikwepa kwa kubonyea chini kidogo kwa umakini mkubwa
alio kuwa nao aliweza kuiona ngumi hiyo inavyo kuja kwa kasi.
Macho ya Agnes yakakutana na macho ya mtu aliye vaa kinyago, huku sura
yake yote ikiwa imefichwa na kinyago hicho cheusi. Mavazi ya mtu huyo
yanarangi nyeusi tupu kuanzia chini hadi juu. Mgongoni mwake amechomeka
sime ndefu iliyopo kwenye sehemu yake maalumu.
“Twende huku”
Hapo
Agnes ndipo aliweza kumtambua mtu huyo ni msichana, hii ni baada ya
kumuambia maneno hayo kwa lugha ya kiswahili sahihi. Agnes akataka
kusita ila binti huyo akamvuta kwa nguvu, wakanza kukimbia wakikatiza
katika kwenye kundi la watu wanao kimbia kimbia pasipo kujielewa.
Kundi
la askari wapatao sita wakasimama mbele yao wakiwa na virungu, Binti
huyo akamuachia Agnes mkono, kwa kasi ile ile walio kuwa wanakimbia
nayo, akajirusha hewani mita nne kwenda juu, huku akijiviringisha kwa
sarakasi, akawapita askari hao kwa juu, akatua nyuma yao nakuwafanya
askari hao kupagawa. Kila askari aliye jaribu kurusha kirungu, aliweza
kukutana na teke zito lililo muangusha chini. Agnes baada ya kuona
msichana huyo anamsaidia, naye akawajibika katika kujibu mashambulizi ya
ngumi zinazo pigwa na askari hao walio chapika kisaswa sawa kama watoto
wadogo.
Ndani ya dakika mbili, hapakuwa na askari aliye weza kusimama, kila mmoaja aliweza kushikilia kiungo alicho weza kuvunjwa.
Kwa
bahati nzuri, kuna treni inayo kwenda kwa mwendo kasi ikawa imefika
katika kituo hicho, abiria wakushuka wakashuka na abiria wakupanda nao
wakapanda. Agnes na binti huyo wakajichanganya na kuingia ndani ya treni
hiyo, hadi askari wanagundua hilo tayari terni hiyo ilisha anza
kuondoka taratibu kwenye kituo hicho. Jambo ambalo liliwawia ugumu
askani ni kuisimamisha terni hiyo kwani kwa mujibu na sheria ya treni
hizo, hazipaswi kusimama pale zinapo ondoka, kutokana kufanya hivyo
kunaweza kusabibisha treni inayo kuja kwenye kitua hicho kuweza
kugongana na kusababisha ajali kukbwa na ubaya zaidi treni hizo huwa
zinatumia dakika tano tano kukaa kwenye kituo.
Kila abiria aliye waona Agnes na mtu huyo aliye valia ninja na kuificha
sura yake, alikaa kimya huku kila mmoja akiwa na woga kwa upande wake,
kwani wanaonekana ni watu hatari.
“Hii sio sehemu salama”
Binti huyo alizungumza huku akichungulia nje ya treni kwa kutumia vioo vilivyopo pembeni.
“Kutoka hapa hadi kituo kingine kuna msitu katikati, itatubidi kutoroka la sivyo kituo kinacho fwata nilazima tutakamatwa”
Sauti ya msichana hiyo ni ngeni masikioni mwa Agnes.
“Tunafanyaje sasa?”
“Twende juu”
“Juu…..!!!”
Agnes
aliuliza huku akiwa amemtumbulia macho binti huyo, kwani mwendo wa
treni hiyo ulivyo mkubwa ni hatari sana mtu kufungua hata kioo..
“Ndio twende juu”
Binti
huyo alizungumza huku akichomoa jambia lake refu, watu wote waliomo
ndani ya behewa hilo wakaka kimya kwani mlio wa kuchomolewa kwake tu,
ulimstua kila mmoja. Binti huyo akapiga hatua mbili mbele kutoka katika
sehemu alipo simama yeye na Agnes.
“KAMA UNAHITAJI KUISHI TOKA NDANI YA HILI BEHEWA”
Alizungumza
kirusi, abiria wote wapatao kumi na tano wakaanza kutafuta ustaarabu wa
kuingia katika mabehewa ya mbele au ya nyuma. Ndani ya dakika wakabaki
wao wawili tu ndani ya behewa hilo.
“Ngoja kwanza wewe ni nani?”
“Hupaswi kunifahamu muda huu”
“Nani aliyeku………….”
Agnes
hakuimalizia sentesi yake, jambia hilo linalo meremeta kama kioo,
likawa limesimamishwa sentimita chache kutoka shingoni mwake.
“Huwa sipendi maswali ya kipuuzi nikiwa kazini”
Agnes
akameza fumba la mate kwani tayari amesha gundua mwanamke mwenzake huyo
ana uwezo mkubwa sana kuliko yeye na endapo atajaribu kupimana naye
uwezo wa kupigana itakula kwake.
“Fwata nitakacho kuambia”
Alizungumza huku alilishusha chini jambia lake hilo, Agnes akashusha pumzi kubwa kwani shingo yake ingegawanyishwa vibaya.
***
Kwa haraka, Rahab akarusha ngumi za kasi zilizo tua shingoni mwa askari
mmoja aliye kuwa kiherehere kuwazuia kuingia ndani ya chumba hicho.
Mwengine kabla hajafanya chochote Raisi Praygod Makuta akampuka kiwiko
cha uso askari huyo nakumfanya mikono yake yote aipeleke usoni mwake
kwani giza la gafla liliyafunika macho yake. Rahab akaingia ndani ya
chumba huku raisi Praygoda akifwatia kuingia
“Mambo mengine munajitakia wenyewe”
Daktari
huyo wa zamu alizungumza huku akimsukumia pembeni askari aliye ufunika
uso wake kwa viganja vyake. Dokta baada ya kuingia ndani ya chumba hicho
na kukuta mashine ya kupumulia inaonyesha mstari mmoja mwenkundu
ikiashiria mgonjwa huyo amefariki, akajikuta amechanganyikiwa.
“Si alikuwa hai huyu”
Daktari
alizungumza huku akijaribu kumminya Samson kifuani mwake. Rahab
akamshika mikono daktari huyo na kumzuia kufanya akacho kifanya
“Tayari ameshakufa ila naomba sindano”
“Sindano………!!!?”
“Ndio sindano”
Daktari huyo akajipapasa pasa kwenye mifuko yake, hakukuta sindano
“Dakika moja”
Akatoka
kwa kasi na kuelekea sehemu ambapo anaamimi nanaweza kupata bomba la
sindano. Rahab baada ya daktari huyo kutoka, akaufunga mlango kwa ndani
na kusimama pembeni ya kitanda alipo simama mumewe.
“Sasa tunafanyaje na mgonjwa amesha kufa?”
Raisi Praygod aliuliza huku akiwa amekata kabisa matumaini yakundelea kukaa ndani ya chumba hicho.
“Ngoja nikuonyeshe kitu ila ninaomba iwe siri yako mume wangu”
“Siri? Kitu, kitu gani?”
“Subiri”
Rahab
akachomoa bastola yake, akatoa magazine. Kwakutimia ncha ya kali ya
chini ya magazine hiyo inayo hifadhia risasi, akajikata kwenye mkono
wake wa kushoto sehemu yenye mshipa wa damu.
“Unataka kufanya nini mke wangu!!?”
“Subiri utaona mume wangu”
Rahab
akamfunua Samson kinywa chake, akaanza kuyanyunyuzia matone ya damu
yake kwenye kinywa cha Samson, baada ya kuridhika kiasi cha damua alicho
kiingiza mdomoni mwa Samson kinatosha, akachanan kipande cha shuka,
akajifunga sehemu ambayo damu inatoka. Akamsogelea Samson karibu,
akampulizia pumzi kiasi Samson. Taratibu vidole vya miguu vya Samson
vikaanza kucheza, ikiashiria uhai wake umesha rudi.
“Samson, Samson, Samson”
Rahab
aliita mara tatu, Samson akayafumbua macho yake, huku macho yake yote
yakiwa mekundu sana. Rahab akamkazia macho Samson, kila walivyo zidi
kutazamana ndivyo jinsi macho ya Samson yalivyo rudi katika hali yake ya
kawaidia. Raisi Praygod Makuya, na ujasiri wake wote akajikuta
akitetemeka kwani tangu azaliwe hakuwahi kusikia kama kuna binadamua
anaye weza kufufua binadamu mwengine.
“Fungu mlango”
Rahab
alizungumza kwasauti nzito kidogo, iliyo mfanya Raisi Praygod
kukimbilia mlangoni, kitendo cha kuufungua mlango dokta wa zamua
akaingia, alipo muona Samson akinyanyuka na kukaa kitako kitandani,
akajikuta akidondosha bomba la sindano. Mwili mzima ukamuishia nguvu
akaanguka chini na kupoteza fahamu.
“Amezimia tu”
Rahab alizungumza huku akimtazama dokta huyo aliye lala sakafuni.
“ASANTE MADAM RAHAB”
Samson alizungumza kwa sauti nzito kiasi, Rahab akaachia taasamu pana akiamini jaribio lake limefanikiwa.
“Niagize chochote nitafanya Madam Rahab”
Samson aliendelea kuzungumza huku akimtazama Rahab aliye simama mbele yake.
“Twende nyumbani sasa”
Rahab
alizungumza. Sasmso akasimama wima akajigeuza geuza akiashiria yupo
safi. Rahab akalishika la hospitalini alilo valishwa Samson, akalichana
kwa nguvu na akabaki tumbo wazi. Hapakuwa na jeraha lolote mwilini mwa
Samson. Raisi Praygod akabaki ameduwaa tuu, kwani kila linalotokea
kwenye macho yake ni kama ndoto. Rahab baada ya kumtazama mume wake
akagundua yupo kwenye hali ya woga. Akasogelea, akanyonya mate, yaliyo
ufanya mwili wa Raisi Praygod kushikwa na kijiubaridi, kilicho utoa woga
wote na kurudi katika hali ya kawaidia.
“Twende zetu Praygod”
“Sawa”
Wakatoka
wakiwa wameongozana na Samson, askari wanao endelea kuugulia maumivu,
baada ya kuona mgonjwa waliye amini ni mahututi akitoka anatembea huku
akiwa hana hata bandeji moja mwilini wake wala kidonda, wakabaki wakiwa
wameduwaa kila mmoja akiwa haamini wanacho kiona.
***
“Muheshimiwa kazi yako nimesha imaliza”
Dokta Maliki alizungumza kwa kutumia simu yake ya mkononi huku akizidisha mwendo kasi wa gari gari lake.
“Unauhakika kama Samson amefariki?”
Makamu
wa raisi alizungumza kwa kufoka sana hadi dokta Maliki akashangaa kwani
si kawaidia ya kiongozi wake huyo kuzungumza kwa sauti ya ukali kama
hivyo
“Ndio muheshimiwa”
“Pumbavu wewee, mtu hajakufaa unaniletea ujinga unjingaa hapaaa”
Makamu
wa raisi alizungumza kwa kufoka, hadi dokta Maliki akajikuta akifunga
breki za gafla, na kusimamisha gari lake pembeni ya barabara
“HAJAKUFAA……!!!?”
“Fala wewe, unamuuliza nani”
Makamu
wa raisi akakata simu. Dokta Maliki akabaki anaishangaa simu yake, kila
alvyo jaribu kuvuta kumbukumbu zake, anakumbuka aliweza kumnyonga
Samson hadi amefariki, sasa inakuwaje makamu wa raisi aseme Samson yupo
hai.
Akiwa
katika dimbwi la mawazo ujumbe wa meseji kupita whatsapp, ukaingia
kwenye simu yake, kwa haraka akaufungua na kukutana na namba ngeni iliyo
tuma picha ambayo bado inaendela kusoma kwa ajili ya kufunguka.
“Comen comennnn”
Dokta
Maliki alizungumza na simu yake hiyo, mara baada ya kuona picha hiyo
inachelewa kufunguka kutokana na mtandao wa internet katika sehemu alipo
kuwa ni mdogo. Picha hiyo ikafunguka hapo ndipo dokta Maliki alipo
amini kwamba Samson yupo hai. Kwani picha hiyo inamuonyesha Samson akiwa
ameongozana na watu watatu ambao alipishana nao mara baada ya kuwaona
wakiingia hospitalini.
“Shitiiiiiii Fuc**………..!!!!!”
Dokta
Maliki alijikuta akipiga mgumi nzito kwenye mskani wake hadi honi ya
gari lake ikalia kwa nguvu. Gafla taa za mbele za gari yake zikafifia
sana, akaiweka pembeni simu yake kwani kufifi kwa taa za gari yake hiyo
mpya aina ya Breves, kilimstua akafungua mkanda wa siti yake, gafla taa
zake zikarudi katika hali ya ukawaida, cha kumshangaza zadia mbele ya
gari lake amesimama mtu aliye mpa mgongo, jambo lililo mtisha Doktar
Maliki.
Akaminya
honi zake kwa nguvu ili mtu uyo kuweza kupisha njiani, na mbaya zaidi
dokta Maliki aligundua amasimama katikati ya daraja la Sarenda. Kwa
haraka akilini mwake akahisi ni majini ambao mara kwa mara inasadikika
yanaonekana kwenye daraja hilo. Akawasha gari yake ila haikuwaka
akajaribu kuliwasha gari lake ila halikuwaka kabisa.
==> ITAENDELEA