test

Jumanne, 22 Novemba 2016

RIWAYA: She is My Wife- Sehemu ya 43 & 44


 Mwandishi: EDDAZARIA G.MSULWA
ILIPOISHIA  
Kwanza kijana huyo akamkumbatia raisi Praygod Makuya, nakumfanya raisi Praygod Makuya kujitahidi kuvuta kumbukumbu zake niwapi alipo muona kijana huyu anaye mwagikwa na machozi. Kumbukumbu za raisi Praygod Makuya zikagota kwenye ndege na kukumbuka kijana huyu ndio yule aliye kuwa akishirikiana na Rahab.
“We…weee si…”  
Raisi Praygod alizungumza kwa kigugumizi, kwani kama kijana huyu alimkosa kwenye ndege basi leo amekuja kumuua kwenye alaiki ya watanzania.
“Samson, Samson muheshimiwa.”
Samson alizungumza huku machozi ya uchungu yakimwagika, akazidi kumkumbatia Raisi Praygod Makuya kwa nguvu zake zote.
                                                                                        
ENDELEA
Raisi Praygod Makuya akajaribu kujitoa mikoni mwa Samson ila akajikuta akishindwa kwani Samson alizidi kumkumbata kwa nguvu
“Naoamba unisamehe muheshimiwaa”
Samson alizungumza huku akiendelea kumwagikwa na machozi mengi. Makamu wa rais baada ya kumuona Samson, ikanyanyuka kwenye kiti chake huku macho yakiwa yamemtoka. Woga wa siri yake kuweza kufichuliwa na mjomba wake huyo ukaanza kumtawala.

“Muheshimiwa natambua kwamba nilikukosea, ila si kosa langu mimi”
“Nilitumwa niweze kukuangamiza, na mjomba wangu ili kiti chako cha uraisi kiweze kukaliwa na mjomba wangu ambaye ni makamu wa raisi wa sasa”
Maneno ya Samson yakamfanya raisi Praygod kuweza kumtazama makumu wa raisi aliye  keti kwenye jukwaa. Sura ya makamu huyo ikamuashiria raisi Praygod kwamba ina hasira dhidi yake.

“Nimekuelewa kijana, unaitwa nani?”
“Samson”
“Sawa Samson nitalifanyia kazi”
“Kabla ya hayo kuna jengine muheshimiwa nahitaji kukuambia”
Makamu wa raisi alipo zidi kumuona Samson anazungumza na Raisi Praygod, akazidi kushikwa na hasira akiamini kwamba kila kitu kimesha haribika, akaangaza macho yake huku na huku, akamuona mlinzi wake aliye simama pembeni, bastola ikiwa imechomekwa kiunoni. Kwa haraka makamu wa Raisi akaichomoa bastola hiyo bila hata yakufikiria mara mbili, akafyatua risasi ambazo kwa haraka Samson aliweza kuliona tukio hilo, alicho kifanya ni kumsukumia pembeni Raisi Praygod, na risasi hizo mbili zikaingia mwilini mwake na kumuangusha chini.

Mlio wa bastola hiyo, ukazua hali ya taharuki kwa kila aliye kuwa katika uwanja wa taifa, kila mmoja akafanya jinsi akili yake ilivyo muagiza kuweza kufanya, wapo walio weza kuchanganya miguu yao na kukimbia hovyo hovyo, wengine waliweza kupoteza fahamu, wengine waliweza kukanyagwa vibaya pale walipo zidiwa nguvu na wale walio hitaji kuokoa nafsi zao. Askari na walinzi wa viongozi waalikwa wakawa na kazi moja tu, yakuwaokoa viaongozi wao waliomo ndani ya kiwana hichi kikubwa cha mpira. Hali ikazidi kuwa mbaya kwani hapakuwa na aliye weza kuvumilia. Walinzi wengi wakamzunguka Raisi Praygod, wakamtoa uwanjani huku wakiwa wanamkimbiza, baadhi ya wanajeshi wakaweza kumtia nguvuni makamu wa raisi aliye weza kufanya tukio lakinyama.

Hali ya Samson, ikazidi kuwa mbaya huku macho yake akimtizama jinsi Raisi Praygod anavyokimbizwa na askari kuyaokoa maisha yake, Samson akaachia tabasamu pana, huku taratibu macho yake yakiingiwa na ukungu ulio pelekea kuyafumba macho yake na kutulia tuli.
                                                                                         ***
     Moja kwa moja Agnes akakimbilai kwenye chumba amacho aliamini kiongozi anaye muhitaji ni lazima atakuwa amepelekwa huko baada ya milipuko hiyo ya magari kuweza kutokea. Akafanikiwa kufika kwenye kordo yakuelekea kwenye chumba hicho kilichopo chini ya ardhi. Walinzi walio valia suti nyeusi pamoja na miwani nyeusi wapatao kumi na tano, wakawa wamesimama nje ya mlango huo huku macho yao yote wakimtupia Agnes anayekuja kwa kasi huku akiwa amejiamini sana.

Kila mmoja akabaki kuwa na alama ya kujiuliza kwani mavazi aliyo yavaa Anges ni ngumu sana kumtilia mashaka kwani akafanana sana na wahudumu wa kikosi cha kuzima moto. Muonekano wa umbo dogo dogo la Agnes, likawapa imani kwamba binti huyo anaye kuja kasi huku akiwa amenyanyau mikono yake juu, hana madhara yoyote kwao.

“Naomba muwatoe viongozi nje, jengo limeanza shika moto”
Kauli ya Agnes aliyo izungumza kwa lugha ya kirasia, ikawafanya walinzi wote kuchanganyikiwa, ikawalazimu kuwasiliana na wezao waliomo ndani ya chumba kuweza kuwatoa viongozi hao haraka iwezekanavyo. Bwana Paul Henry Jr pamoja na Raisi wa Russia wakatolewa ndani ya chumba hicho kuku wakiwa wamezungukwa na walinzi wao wapatao ishirini.

“GO GO GO….!!!”
Mlinzi mmoja alizungumza huku akionekana ndio mkuu wa kikosi hichi maalumu chakuwalinda viongozi hawa. Agnes akatazama jinsi walinzi hawa walivyo makini na kuwalinda viongozi hawa.
“Hapa hapa”
Agnes akawaacha viongozi hao kupiga  hatua nyingi mbele, kisha  kwa kasi akanza kukimbia na kuwafwata kwa nyuma, akamfikia mmoja aliye ishika bastola yake na kuitanguliza mbele. Kwa kasi ya ajabu Agnes akajigeuza kwenye shingo ya mlinzi huyo na kuivunja, kabla hajaanguka chini, tayari akawa ameikamata bastola ya mlinzi huyo.

Kwa mafunzo ya uharaka na umahiri wake katika kutumia silaha hizi za bunduki, Agnes, akaanza kuwaangusha chini walinzi hao, walio changanyikiwa kwani, kitendo cha mtu kujaribu kufanya shambuliza tayari umesha vamiwa na kuangushwa chini.
Agnes akafanikiwa kusimama nyuma kwa bwana Paul Henry Jr, akampiga kabali huku bastola yake akiwa ameiweka sikioni mwa kiongozi huyo. Macho yake kwa haraka aliweza kuona miili ya walinzi wapatao kumi na sita wakiwa chini wamekufa huku wanne wakiwa wamesimama huku wamenyooshea bastola zao.


Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx