Naibu Kamishna mstaafu wa Magereza nchini (DCP), Luhusa Chiza (62) amefariki dunia katika mazingira ya utata kwenye Hoteli ya Kitemba mjini Dodoma.
Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo, mwili wa Chiza uligunduliwa juzi
mchana na mmoja wa wahudumu wa hoteli hiyo alipotaka kufanya usafi.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji, zilidai Chiza aliingia Novemba 15 usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye.
Taarifa zaidi kutoka ndani ya hoteli hiyo iliyopo Barabara ya Sita katikati ya mji, zilidai Chiza aliingia Novemba 15 usiku na msichana ambaye alitoroka baadaye.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro
Mambosasa alisema mwili wa Chiza ulikutwa ukiwa na damu puani na kwamba,
aliingia chumbani akiwa na msichana ambaye wanamtafuta.
Alisema
kamishna huyo alifika mjini hapa akitokea jijini Dar es Salaam kwa
ajili ya kukagua viwanja vyake na kwamba, alikuwa akielekea mkoani
Kigoma.
Meneja wa Hoteli ya Kitemba, Crispin Daniel alisema mteja huyo aliingia Novemba 15.
Meneja wa Hoteli ya Kitemba, Crispin Daniel alisema mteja huyo aliingia Novemba 15.
“Mhudumu alikuja kuniambia kuna mteja hajisikii
vizuri chumbani, anatapika si kwamba alifariki dunia akiwa hapa.
Ingekuwa hivyo usingekuta hivi,” alisema.
Alisema baada ya kupokea
maelezo hayo, alipiga simu polisi na walifika na kumchukua na hafahamu
kilichoendelea.
“Watu wanasema alifia hapa kwa sababu waliona polisi
wamejaa, ukweli alitoka akiwa anaumwa ndicho ninachofahamu,” alisema.
Kaimu Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Dodoma, Dk Caroline Damian
alithibitisha kupokewa kwa mwili huo juzi mchana.
“Tayari tumeshamfanyia
postmortem (uchunguzi) na tumechukuwa sampuli ya chakula, kwa ajili
ya kupeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali,” alisema.
Mkuu wa Magereza Mkoa
wa Dodoma, Antonio Kilumbi alisema mwili wa ofisa huyo ulisafirishwa
jana kwenda Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma kwa mazishi.
“Alikuwa akitokea Dar es Salaam kuchunguza afya yake maana anapressure (shinikizo la damu) na alishawahi kuzimia mara nyingi tu,” alisema Kilumbi.
“Alikuwa akitokea Dar es Salaam kuchunguza afya yake maana anapressure (shinikizo la damu) na alishawahi kuzimia mara nyingi tu,” alisema Kilumbi.