Kile kikundi cha kigaidi kijulikanacho na kuogopwa kwa ukatili wa
kutisha hili kuleta hofu kimeenda hatua zaidi mbele kwa kuweka sheria
kali.
Wahuni hao Wamepiga marufuku uvaaji wa boxer na Chupi kwa wanaume
kwasabab ni kimagharibi badala yake unatakiwa uvae bukta ndefu inayovuka
magotini ama kitambaa unachojifunga kiunoni kama taulo. Na ukibainika
kuvaa hivyo hatua kali itachukuliwa dhidi yako.
Wanajeshi wa Iraq na Kurd walishangaa kukuta mabandiko hayo yanayokataza
uvaaji wa Chupi na Boxers walipoukomboa mji wa Hammam Al Allil kusini
mwa Mosul dhidi yao.
Pia ISIS imepiga marufuku kunyoa ndevu, kusikiliza mziki na kuvaa jeans zilizobana.