Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema leo amefikishwa tena Mahakama Kuu Kanda ya Arusha kwa ajili ya kusikiliza rufaa yake ya maombi ya dhamana.
Ulinzi
ulikuwa umeimarishwa mahakamani hapo huku wafuasi wa Lema wakiwa
wamevaa fulana nyeupe zilizoandikwa Jutice 4 Lema mbele zikiwa na picha
yake.
Mbele
ya Jaji Fatma Masengi aliyekuwa amepangwa kusikiliza Rufaa hiyo,
Upande wa Jamhuri ambao ulikuwa ukiwakilishwa na mwanasheria Matenus J
Marandu umeweka pingamizi kwamba mawakili wa Lema walipaswa kupeleka
notisi ya rufaa kwanza na siyo kukata rufaa
Wakili
wa Chadema Peter Kibatala amesema wao wameshakamilisha taratibu zote za
kisheria, hivyo wanasubiri uamuzi wa pingamizi hilo lililowekwa na
upande wa serikali.
Jaji
Fatma Masengi ameutaka upande wa serikali uwasilishe hoja za pingamizi
lao kwa njia ya maandishi kabla ya November 30 ili aweze kutolea
uamuzi December 2 mwaka huu.
Ulinzi ukiwa umeimarishwa