Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Philip Mpango amezindua rasmi bodi ya wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo TIB kwa kuiagaiza iweke mikakati yakutaua changamoto mbalimbali zitakozoiwezesha kushiriki kikamilifu katika utelezaji wa Mpango wa pili wa maendeleo wa miaka mitano.
Bodi hiyo imeundwa kufuatia uteuzi wa Mheshimiwa Rais, Dkt. John Pombe Magufuli uliofanyika mwezi Julai 2016.
Akizindua
bodi hiyo, Dkt. Mpango aliwakumbusha wajumbe kufanya kazi kwa ufanisi
na weledi ili kuweza kufanikisha azma ya Rais ya kujenga Tanzania ya
Viwanda.
“Serikali
ya awamu ya tano imejikita kwenye kuhakikisha kuwa uchumi wetu unakuwa
ni uchumi wa viwanda. Benki hii ikiwa ni benki ya kisera inawajibu wa
kuhakikisha hili linatekelezwa. Kwa mantiki hiyo ni matarajio ya
serikali kuona kuwa benki inachochea maendeleo katika nyanja zote muhimu
za uendelezaji wa viwanda vya kuzalisha umeme na miundombinu yake,
maji, barabara/usafirishaji na mawasiliano ili kufikia malengo tarajiwa
hususan kuhakikisha kuwa Tanzania inakuwa ni nchi ya uchumi wa kati
unaotegemea viwanda ” alisema Dkt. Mpango.
Kwenye
maelezo yake ya awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo TIB,
Charles Singili mbali na kuainisha juhudi zinazofanywa na benki hiyo
katika kutekeleza mipango ya maendeleo ya Taifa alielezea changamoto
mbalimbali zinazoikabili benki hiyo. Changamoto hizo ni pamoja na udogo
wa mtaji, uhitaji wa kuwepo kwa fedha za kuandaa miradi, taratibu ndefu
za upatikanaji wa vibali vya kukopa kwa taasisi za Serikali na uwepo wa
mikopo chechefu.
Waziri Mpango pia aliongelea changamoto zinazo ikabili benki hiyo ikiwemo suala la mtaji ambapo alisema, “Serikali
ya awamu ya tano inalifanyia kazi suala hili ili kuleta suluhisho
endelevu na kuiwezesha benki hii kutimiza malengo ya kuundwa kwake”.
Pia
aliisisitizia bodi kuweka mikakati madhubuti katika kukusanya madeni,
kusimamia mikopo inayotolewa na kuhakikisha kuwa mikopo inayoidhinishwa
ni kwa miradi inayo stahili na yenye uwezo wa kurejesha mikopo hiyo.
Aidha, aliitaka benki hiyo kutokufanya kazi kwa mashinikizo yoyote kutoka kwa watu, wanasiasa, idara au taasisi yoyote; bali wazingatie sheria, kanuni na taratibu zinazoongoza tasnia ya mabenki kama zinavyoelekezwa na Benki Kuu ya Tanzania.

Kwa
upande wake, Mwenyekiti mpya ya bodi hiyo ilioteuliwa Profesa
Palamagamba John Kabudi alimuahidi Waziri kuwa watafanya kazi kwa weledi
wa hali ya juu na kutekekeleza maelekezo aliyoyatoa ili kutimiza
matarajio ya Serikali na waliowateua.
Aidha, Mwenyekiti Profesa Kabudi alisema “Tutafanya jitihada ya kutafuta ufumbuzi wa changamoto mbalimbali zinazo ikabili benki yetu, Kwa yale yanayohitaji maelekezo ya ofisi yako hatutasita kuwasiliana na ofisi yako na yale yaliyoko ndani ya mamlaka yetu tutayashughulikia kulingana na taratibu za kiutendaji katika sekta husika.”

Bodi
hiyo iliyozinduliwa rasmi mjini Dodoma sasa itaanza kazi zake rasmi
kuhakikisha inaiendeleza na kuiimarisha Benki hiyo ya Maendeleo TIB.