test

Jumamosi, 15 Oktoba 2016

Waliosekwa rumande na DC watoka na kulipa madai


WATUMISHI watatu walioswekwa rumande na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza, Emmanule Kipole, akiwemo Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Oscar Kapinga wametoka rumande na kutekeleza agizo walilopewa na mkuu huyo wa wilaya.

Kaimu Mkurugenzi pamoja na Kaimu Mweka Hazina wa Wilaya, Paul Sweya na Mhasibu Hassani Moshi waliswekwa rumande kwa amri ya Mkuu wa Wilaya Jumatano iliyopita baada ya kukaidi agizo la kuwataka wawalipe wafanya usafi wa mji wa Sengerema waliokuwa wameandamana hadi katika ofisi za halmashauri hiyo.
Watumishi hao juzi saa 4 asubuhi waliachiwa kutoka rumande ya Kituo cha Polisi Wilaya ya Sengerema kisha kwenda kuwalipa wafanya usafi kiasi cha Sh 29,000 kila mmoja ingawa fedha hizo hazikukidhi kiu ya wafanya usafi hao.
Utekelezaji wa kuwalipa watu hao ulifanyika saa 10 jioni muda mfupi baada ya watumishi hao kuachiwa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx