Taasisi
na Mashirika ya Umma nchini yametakiwa kujiendesha kwa faida huku
yakiwa na mtazamo wa kiushindani na makampuni yaliyo chini ya sekta
binafsi na kwamba hakuna sababu yoyote kwa mashirika hayo kuendeshwa kwa
hasara na kugeuka mzigo kwa serikal
Msajili wa Hazina nchini Bw. Lawrence Mafuru ametoa agizo hilo jana
jijini Dar es Salaam wakati akisaini makubaliano ya kiutendaji na
taasisi 12 za umma, mkataba unaohusisha malengo ya uendeshaji, namna ya
kuhudumia wananchi sambamba na usimamizi bora wa rasilimali za umma
zilizopo ndani ya mashirika hayo.
Zoezi
hilo la linafanya idadi ya taasisi ambazo msajili wa hazina amesaini
nazo makubaliano kufikia thelathini tangu aanze utaratibu huo unaoendana
na falsafa ya serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha kunakuwa na
uwajibikaji katika taasisi na mashirika ya umma.
Katika
maelezo yake Bw. Mafuru amesema haikubaliki kuona makampuni na taasisi
za umma zikiendelea kupata hasara kwa kutekeleza majukumu yale yale
ambayo taasisi na makampuni binafsi yanapata ufanisi na faida pasipo
visingizio vyovyote.