test

Ijumaa, 14 Oktoba 2016

Nyangumi akutwa amekufa ufukweni mwa Bandari ya Kilwa


SAMAKI Mkubwa aina ya Nyangumi amekutwa leo akiwa amekufa katika ufukwe wa Bahari ya Hindi eneo la Bandari ya Kilwa, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Ripiti kutoka eneo la tukio zinasema Nyangumi huyo alianza kuonekana akielea baharini tangu jana na leo alfajiri alisukumwa hadi ufukwe huo katika bandari ya wavuvi.

Mmoja wa wananchi katika eneo hilo, Akram Kidudu ameiambia Habarileo Online kuwa bado haijajulikana chanzo cha kifo cha nyangumi huyo na polisi wapo eneo la tukio kuzuia wananchi wasianze kugawana kitoweo hicho bila kujua usalama wake.
CHANZO:HABARI LEO

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx