MPWAPWA, DODOMA: Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwanamme mmoja ambaye hajajulikana jina anayedaiwa kuwa ni mfanyabiashara katika stendi ya mabasi ya Mpwapwa mkoani Dodoma amejichinja kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Amejikata koromeo kwa kutumia kisu baada ya mwanamke aliyekuwa naye kumkataa kwa madai kuwa ana mwanamme mwingine
Inaelezwa kuwa mwanamke huyo pamoja na mwanamme anayedaiwa kuchukua mpenzi wa mwanamme aliyejichinja pia wanafanya kazi katika stendi hiyo ya mabasi.
Wasamaria wema walimkimbiza hospitali hospitali ya wilaya ya Mpwapwa kwa ajili ya matibabu baada ya tukio hilo