Mshtakiwa huyo ambaye hadi kupandishwa kizimbani, kulizuka hali ya sintofahamu kwa waandishi wa habari, ambapo wakati kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei, akisubiriwa kuonana na waandishi wa habari waliotaka ufafanuzi kuhusu kukamatwa na kuwekwa ndani kwa mkurugenzi huyo tangu Oktoba 15 mwaka huu, askari polisi walimtoa kwa siri mtuhumiwa na kumpeleka mahakamani bila taarifa hizo kuwekwa wazi.
Imedaiwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo Agripina Kimaze, na waendesha mashtaka wa serikali, Sunday Hyera na Edgar Bantulaki kuwa, mshtakiwa katika shtaka la kwanza analodaiwa kutenda Oktoba 15 mwaka huu, inadaiwa amemtishia kumuua kwa bastola askari namba 5057, Coplo Tuti Ndaga wa kikosi cha usalama barabarani mkoa wa Morogoro, huko maeneo ya Mbuyuni Mkambalani katika wilaya ya Morogoro.
Katika shtaka la ukiukwaji wa sheria za usalama barabarani, lenye makosa mengine matano, inadaiwa siku hiyo huko Mbuyuni Mkambalani, mshtakiwa aliendesha gari namba T 845 CTJ aina ya Prado bila kuwa na leseni, bima, mwendo kasi wa spidi 85 badala ya 50 zilizoruhusiwa eneo hilo, huku akidaiwa kukataa kupeleka gari kituo cha polisi kilicho jirani kama alivyoamuriwa na askari, WP 5392 Sajent Anna na kosa jingine akadaiwa ni kusimamisha gari katikati ya barabara kwa uzembe, bila uangalifu na kuzingatia watumiaji wengine wa barabara.
Mkurugenzi huyo wa Mkinga amekana mashtaka yote yanayomkabili, ambapo hakimu Kimaze, ameahirisha shauri hilo hadi Oktoba 31 mwaka huu ambapo usikilizwaji wa awali utaanza huku mshtakiwa akiachiwa kwa dhamana baada ya kukidhi masharti ya kuwa na mdhamini mmoja kwa kila kosa, kwa makosa yote mawili ya jinai na lile la usalama barabarani, kwa kutii wadhamini wote wawe kuwa wakazi wa Morogoro, mmoja akitakiwa kuweka dhamana ya shilingi laki tano na mwingine shilingi milioni moja.
============================
Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mkinga mkoani Tanga,Emmanuel Barnabas Mkumbo, anashikiliwa na jeshi la polisi mkoani Morogoro baada ya kujifanya Usalama wa Taifa nakumtishia kwa Bastola askari wa usalama barabarani wakati wakielekea kituo kidogo cha polisi kingoluwira, alikotaka apelekwe kuzungumza na mkuu wa kituo baada ya kukamatwa akiwa amezidisha mwendo kasi (Speed)
Tukio hilo limetokea barabara kuu ya Morogoro - Dar es salaam