test

Jumatatu, 17 Oktoba 2016

Mkurugenzi Misungwi amdhalilisha mwalimu mbele ya wanafunzi wake


Mkurugenzi halmashauri ya wilaya Misungwi amemdhalilisha mwalimu wa shule ya Sekondari Shilala iliyopo Wilayani humo baada ya kumuamrisha kudeki darasa huku wanafunzi wake wakimshuhudia
Tukio hilo lilitokea pale ambapo Mkurugenzi huyo akiwa ameambatana na baadhi ya mafisa walipo fika shuleni hapo mida ya jioni, muda ambao wanafunzi wa kidato cha nne walikuwa wakijisomea ili kujiandaa na mitihani.

Alipofika sekondari hiyo ya Shilala alitembelea madarasa baadhi na kukuta darasa moja likiwa chafu, ndipo akamuhitaji mwalimu aliye karibu kuja kujibu kwa nini darasa chafu na baada ya hapo mkurugenzi huyo akamwamrisha mwalimu huyo kudeki darasa hilo jambo ambalo mwalimu huyo hakuwa na pingamizi ingawa mwanzo alidhani huenda anaambiwa awaambie watoto wasafishe, hivyo akawa anafanya mpango wa kuwaambia wanafuzi ndipo mkurugenzi bila hata chembe ya busara akamwambia udeki wewe mwenyewe, mwalimu hakuwa na ajizi akatafuta ndoo na maji na kuanza kudeki huku wanafunzi wakimshuhudia.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx