Mfalme wa Morocco Mtukufu Mohammed VI jana tarehe 27 Oktoba, 2016 ameondoka Jijini Dar es Salaam na kuelekea Zanzibar.
Katika
Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed
VI aliagwa na Mwenyeji wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Dkt. John Pombe Magufuli aliyeambatana na Makamu wa Rais Mhe. Samia
Suluhu Hassan.
Akiwa
Jijini Dar es Salaam Mtukufu Mohammed VI aliyewasili nchini tarehe 23,
Oktoba 2016 kwa ziara ya kiserikali ya siku tatu amekutana na kufanya
mazungumzo na mwenyeji wake Rais Magufuli na pia viongozi hao
wameshuhudia utiaji saini wa mikataba 21 inayohusu ushirikiano wa
Tanzania na Morocco katika masuala mbalimbali ya kiuchumi.
Baada ya kumaliza ziara ya kiserikali ya siku tatu, Mtukufu Mohammed VI anaendelea na ziara binafsi hapa nchini.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU