Kufuatia mauaji ya kinyama kwa watafiti wa Udongo na Maendeleo ya Ardhi yaliyofanywa na wanakijiji wa Iringa Mvumi wilaya ya CHAMWINO Mkoani DODOMA Mkuu wa wilaya ya Tabora Aggrey Mwanry amevitaka vyombo vya ulinzi na usalama mkoani Tabora kuhakikisha wafanyakazi wa NIDA wanafanya kazi katika hali ya usalama.
Mwanry ameyasema hayo wakati akizindua rasmi zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa kwa watumishi wa umma ambalo linafanyika katika maeneo yote ya mkoa wa Tabora huku akiwahakikishia usalama watumishi wa mamlaka ya hiyo
Nao wakuu wa wilaya za mkoa wa Tabora wamewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutoshai katika zoezi hilo
Zoezi la usajili wa vitambulisho vya Taifa limeanza rasmi kwa kwa watumishi wa umma na baadae kwa wananchi wa kawaida ambapo kwa mkoa wa Tabora litafanyika kwa siku kumi na nne.

