test

Jumanne, 4 Oktoba 2016

Wajumbe wanne wa Bodi ya wadhamini CUF wanaandaa kutatua Mgogoro ulioibuka



Wajumbe wanne wa Bodi ya wadhamini wa chama cha wananchi Cuf kati ya wanane wanaandaa utaratibu wa kuwakutanisha katibu Mkuu wa chama cha wananchi Cuf pamoja na M/kiti wa chama hicho Prof.Ibrahim Lipumba ili kuwapatanisha kutokana na mgogoro ulioibuka ambao unaendelea kukigawa chama hicho.
Wakizungumza na waandishi wa habari jijini dsm wajumbe hao wa Bodi ya Cuf wanne kati ya watano kutoka Tanzania Bara wamesema wanahuzunishwa na Mgogoro wa uongozi ndani ya chama hicho huku pia wakitahadharisha kutomshambulia msajili wa vyama vya siasa kwa kuwa alifuata taratibu,kanuni na katiba ya cuf katika kutoa maamuzi kuhusu mgogoro wa chama hicho.
Aidha wajumbe hao wa bodi wamesema Prof.Lipumba ambaye ni m/kiti wa Chama hicho hawezi kufunguliwa mashitaka,kwa kuwa katiba ya Cuf inabainisha kuwa bodi ndiyo inayoweza kushtaki au kushtakiwa.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx