test

Jumanne, 4 Oktoba 2016

Serikali kuhakikisha inalinda michango ya mfuko wa maafa kwa ajili ya wakazi wa mkoa wa Kagera


Serikali imewahakikishia watanzania na wasamalia wema wanaoendelea kuchangia katika mfuko wa maafa kwa ajiri ya wakazi wa mkoa wa kagera na mikoa ya jirani walioathirika na tetemeko la ardhi kwamba serikali itaendelea kuilinda michango yao ili ifanye kazi iliyokusudiwa.

Waziri Mkuu Kassim majaliwa amesema hayo katika hafla ya kupokea michango kwa ajili ya waaathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera ambapo makampuni zaidi ya 17 yamewasilisha michango yao ya vifaa na fedha zaidi ya shillingi million mia sita.

Pia waziri mkuu amesema serikali inaendelea na uchunguzi wa kubaini nani alikuwa akichukua pesa katika akaunti bandia iliyofunguliwa na baadhi ya watumishi wa umma kwa ajili ya kukusanya michango ya maafa.
Nao baadhi ya wasamalia wema na makampuni waliochangia misaada hiyo wamewataka watanzania wengine kujitokeza na kuchangia maafa hayo kwani hakuna sababu yakusubiri msaada kutoka nje.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx