test

Jumanne, 4 Oktoba 2016

AMETISHA! : OMOG AMPA DARASA KOCHA PLUIJM.



Kocha Mcameroon wa Simba SC, Joseph Marius Omog amekataa kumzungumzia refa Martin Saanya, lakini amesema anakwenda kuwanoa zaidi vijana wake, ili waendeleze rekodi ya kutofungwa katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba SC juzi ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na mahasimu wake wa jadi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Na akizungumza juzi mjini Dar es Salaam, Omog alisema kwamba baada ya matokeo hayo wanarudi kambini kujiandaa na michezo ijayo. “Tunakwenda kuendelea kujituma na mazoezi, ili tuwe katika ubora wetu na kuendeleza rekodi yetu nzuri katika Ligi Kuu,”alisema kocha huyo wa zamani wa Azam FC.
Akiuzungumzia mchezo wa jumamoi, Omog alisema ulikuwa mkali ambao ulikutanisha timu mbili kubwa zenye wachezaji wakiubwa pia. “Tulikuwa pale kwa ajili ya kushinda, lakini malengo hayakutimia,”alisema Omog aliyewahi kufundisha AC Leopard ya Kongo Brazzaville na kuipa Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2012.
Hata hivyo, kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Cameroon, alikataa kulizungumzia bao la Yanga lililotaka kuvuruga amani Uwanja wa Taifa juzi – na kwa ujumla hakutaka kumjadili refa, akisemaa; “Sina maelezo” baada ya kutakiwa kuzungumzia uchezeshaji wa refa na bao la wapinzani wake.
“Hatukushinda kwa sababu tulikutana na timu bora yenye uzoefu mzuri,”alisema Omog ambaye Azam FC watamkumbuka kwa ubingwa wa Ligi Kuu msimu wa 2013/2014.
Hakika kocha Omog ni mfano wa kuigwa, hii ni hekima ya hali ya juu ambayo inapaswa kuigwa na makocha wote Tanzania.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx