Utekelezaji wa mradi huo wa kampuni ya mawasiliano nchini
humo utapanua huduma za mawasiliano ili kuweza kuwafikia watu wengi zaidi na
hivyobasi kuimarisha uchumi.
''Tunawapongeza kwa kutekeleza mradi huu na tunatumai
upandaji wa miti katika maeneo tofauti mjini ikiwemo maeneo ya burudani, watu
wataweza kupata huduma ya mtandao'' ,alisema.
Kwa upande wake Kamishna wa Jimbo la Dar es Salaam Paul
Makonda amesema kuwa mradi huo ni mmoja wa awamu tano za juhudi za serikali
kuimarisha huduma kadhaa hususan mawasiliano na huduma za mtandao kwa wote.
Utekelezaji wa mradi huo ndio mwanzo wa safari ya kujenga
miji na miji mikuu katika kiwango cha 'Smart City' nchini Tanzania.

