WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa mwezi mmoja kwa watumishi waliohamishiwa wilaya mpya ya Kibiti mkoani Pwani kuripoti katika kituo chao cha kazi na watakaoshindwa kutekeleza watakuwa wamejifukuzisha kazi.
Amesema
mtumishi yeyote aliyehamishiwa wilaya hiyo ambaye anaishi nje ya Kibiti
anatakiwa arudi na kuishi kwenye makao makuu ya wilaya na si
vinginevyo.
"Tayari
nimemuagiza ndugu Zuberi Samatabu Katibu Tawala wa mkoa wa Pwani
kuhakikisha anasimamia watumishi wote wa wilaya hiyo wanaoishi nje ya
wilaya hiyo waishi Kibiti na si Ikwiriri," amesema.
Kauli
hiyo ya Waziri Mkuu ilifuatia taarifa ya Mkurugenzi Mtendaji wa
Halmashauri ya wilaya hiyo Alvera Ndabagoye ambaye alimueleza Waziri
Mkuu kuwa ni watumishi wanane pekee kati ya 74 waliopangiwa kufanya kazi
kwenye wilaya hiyo wameripoti katika kituo cha kazi
Ili
kukabiliana na tatizo la uhaba wa nyumba za watumishi amemuagiza Mkuu
wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuzungumza na watendaji wa
mifuko ya hifadhi ya jamii kwenda wilayani huko kuwekeza katika miradi
ya ujenzi wa nyumba za watumishi.
Waziri Mkuu ametoa agizo hilo jana Jumatano,
Septemba 28, 2016 wakati akizungumza na watumishi wa wilaya hiyo katika
ziara yake ya kukagua shughuli za maendeleo,utendaji wa serikali na
kutoa msimamo wa serikali kuhusu utekelezaji wa majukumu yake ya kila
siku
Wakati
huo huo Waziri Mkuu amewataka madiwani wa halmashauri hiyo wawe wakali
katika kusimamia miradi ya maendeleo na kuacha tabia ya kuomba omba kwa
wakuu wa idara ili kuepuka kujishushia hadhi zao na kupelekea kuhujumiwa
kwa miradi mbalimbali ya jamii
Aidha
aliwataka viongozi wa wilaya hiyo kutengeneza mazingira ya kukaribisha
wawekezaji na wahakikishe kwamba uwekezaji utakaofanyika hausababishi
migogoro ya ardhi kwa wananchi.
Waziri
Mkuu amewahamasisha wananchi kuhakikisha wanapeleka watoto shule kwa
maana Serikali imebeba mzigo wote wa gharama za ada na uendeshaji wa
shule hizo.
Alisisitiza
kuwa njia pekee na ya haraka kuondoa umaskini ni kusomesha watoto
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu ameagiza halmashauri zote nchini
kutumia mfumo wa kieletroniki katika ukasanyaji wa mapoto ili kuziba
mianya ya uvujaji mapato haswa ya maliasili