Wizara ya elimu, Sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi imezifuta shule
za awali, msingi na sekondari nchini zaidi ya 40 ambazo hazijasajiliwa.
Kaimu Mkurugenzi wa Usajili wa shule katika wizara hiyo, Khadija
Mcheka, alisema Mei mwaka huu baada kuzipa miezi miwili shule ambazo
hazijasajiliwa kufanya hivyo, walizifungia shule nyingine 12.
Shule zilizofungiwa kwa kuendesha shughuli zake bila usajili
zilitajwa kuwa ni shule za awali na msingi za Must Lead ya mkoa wa
Pwani, na za mkoa wa Dar es Salaam ni Brainstorm, Pax, Lassana, Grace,
Rose Land, Julius Raymod, St Thomas, Mary Mother of Mercy, Noble
Sinkonde, Immaculate Heart of Mary, St Columba, Corner stone, Dancraig,
Mwalimu Edward Kalunga, Edson Mwidunda, Gisela, Kingstar, St Columba
awali, Bilal Muslim, Thado, Hocet , Elishadai, Lawrance Citizen,
Comrade, Dar Elite Preparatory na Golden Hill Academy na Hekima.
Nyingine ni Pwani Islamic, St Kizito na Rwazi Encysloped za Kagera,
Dancraig na Qunu za Pwani, Hellen’s ya Njombe, Joseph ya Arusha,
Samandito na Maguzu za Geita. Alizitaja shule za Sekondari zilizofungiwa
kwa sababu hiyo kuwa ni Hananasif, Elu, Hocet, Safina za Dar es Salaam
na Namnyaki ya Iringa.
“Baada ya kutoa tangazo kutokana na kubaini kuwapo shule nyingi
zisizosajiliwa, wapo waliojitokeza na nyingine tumezifungia kutokana na
kutokidhi viwango vya usajili lakini pia tunaamini wapo waliojificha
wakiendelea kutoa huduma,” alisema Mcheka.
Aliwaagiza wakaguzi katika kanda na wilaya, kufanya ukaguzi na kutoa
taarifa kwa zile ambazo hazijafungiwa na ikithibitika hazijasajiliwa,
kuzifungia mara moja.