MOROGORO: Aliyekuwa mtangazaji wa Channel Ten, kipindi cha Utalii Tanzania, Cassius Mdami amefariki dunia jana katika Hospitali ya Mazimbu Morogoro.
Marehemu alianza kusumbuliwa na maradhi tangu mwanzoni mwa mwaka huu na kupatiwa matibabu jijini Dar es Saalam kabla ya kuhamishiwa mkoani Morogoro, ambako alifikwa na mauti jana mchana akiwa amelazwa hospitali ya Mazimbu iliyopo mkoani Morogoro.
Marehemu enzi za uhai wake alikuwa akitangaza kipindi cha Utalii kinachorushwa na kituo cha luninga cha Chanel Ten, ambacho kwa kiasi kikubwa kimechangia kukuza sekta ya utalii nchini.
Bwana alitoa na bwana ametwaa, Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi.