Salome
ya Diamond imezidi kupata heshima kubwa ndani na nje ya nchi na
inawezekana ikawa ni tofauti na mwenyewe alivyotegemea. Msanii wa muziki
wa asili, Mrisho Mpoto amedai kufurahishwa na wimbo huo kutokana na
kuwa na ladha ya Tanzania.
Mpoto
amediriki kusema hayo kupitia mtandao wake wa Instagram wikiendi hii
huku akiendelea kwa kumpongeza msanii huyo kwa kuutangaza muziki wa
Bongo Fleva na kuiletea heshima Tanzania.
“Nassibu
kiukweli nimefurahishwa sana na kazi yako ya #Salome imeonyesha ukomavu
Mkubwa na team work, kikubwa ukiwa unafanya kazi zenye test ya nyumbani
unatupa heshima kama nchi na inakuonyesha wewe ni nani? na nani siyo
wewe?,” ameandika Mpoto kwenye mtandao huo.
“Nassibu
Mwenda kwao siku zote haogopi Giza, nenda lakini waambie nna kwetu,
kama ulivyofanya kwenye Salome. Sisi ni wabantu bwana tunaruhusiwa zaidi
ya mmoja, na Mimi ntamtafuta Salome wangu wa ukubwani ashike magoti
nisimame kama ngongoti japo nna kitambi ntainama kidogo!!.”
Mpaka sasa video ya wimbo huo imeshatazamwa mara zaidi ya milioni mbili ndani ya wiki moja tangu itoke.