WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amekutana na wawekezaji wa kampuni tisa za nchini
Korea Kusini na kumuahidi kushirikiana na Serikali ya Tanzania kuwekeza
katika sekta ya kilimo, viwanda, maji, miundombinu, elimu, afya na
michezo.
Wawekezaji
hao wanatoka kampuni ya Sima textile, ESM, Jusung Solar Engineering,
Seongnam City FC, Yeong Yang City Korea,Ulsan Vocational Training, Egis
Smart City, MBN
Akizungumza
na wawekezaji hao jana jioni (Jumanne, Septemba 27, 2016) kwa niaba ya
Mhe. Rais Dk. John Magufuli, Waziri Mkuu alisema kwamba Tanzania ni
sehemu salama kwa uwekezaji ikiwa na fursa za uwekezaji kwenye sekta
nyingi kama miundombinu, kilimo na viwanda. Licha ya mazingira mazuri ya
uwekezaji pia aliwahahakishia ulinzi kwenye uwekezaji wao.
Waziri
Mkuu alisema Korea ya Kusini inashirikiana vizuri na Tanzania hivyo
wanatarajia mengi kutoka nchini huko kupitia wawekezaji hao.
Wawekezaji
hao tayari wamefanya mazungumzo na viongozi wa Halmashauri ya Manispaa
ya Ilemela jijinii Mwanza na kusaini Hati ya Makubaliano (MoU) kwa ajili
ya miradi minne ikiwemo ya ujenzi wa miundombinu ya maji, kiwanda cha
nguo, zana kubwa za kilimo na mafunzo ya ufundi.
Kwa
upande wake Mkuu wa Msafara huo, Bw. Son Young Soo alisema
amefurahishwa na ziara waliyofanya nchini na wapo tayari kuwekeza
nchini.
Naye,
Bw. Jihyun Kim wa kampuni ya Yeong Yang City Korea ambayo
inashughulikia masuala ya kilimo cha mbogamboga alisema watawekeza
kwenye kilimo hususan cha zao la pilipili na watajenga kiwanda kwa
ajili ya usindikaji.
Naye
Mkurugenzi wa Klabu ya Soka ya Seongnam Bw. Suk Hoon Lee alisema klabu
yake ipo tayari kuwekeza katika shule ya michezo kwa vijana ili kuongeza
kasi ya maendeleo ya soka.