Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA leo Septemba 21 2016 limetangaza mabadiliko maalum ya michuano ya kombe la mataifa ya Ulaya (EURO2020) litakalofanyika mwaka 2020, UEFA wametangaza mabadiliko ya sehemu ya michuano hiyo itakayofanyika.
Tofauti na miaka ya nyuma michuano hiyo huwa inachezwa katika taifa moja ambalo huchaguliwa mapema na kuwa mwenyeji, safari hii michuano ya Euro 2020 itafanyika katika miji 13 barani Ulaya, lengo likiwa ni kusherehekea miaka 60 ya michuano hiyo.
Mwaka 2020 michuano ya Euro itakuwa inatimiza miaka 60 toka kuanzishwa kwake mwaka 1960, ni miji 13 ya nchi 13 barani Ulaya ambayo itakuwa mwenyeji, miji iliyotajwa ni Munich, Baku, Rome, St Petersburg, Brussels, Copenhagen, Budapest,Amsterdam, Dublin, Bucharest, Glasgow, Bilbao na London.