Taarifa kutoka nchini China juu ya Darubini kubwa zaidi duniani ambayo leo Sepetember 25, 2016 imeanza uchunguzi wa sayari na nyota katika mkoa wa Guizhou ulioko kusini magharibi mwa China.
Leo mchana, mamia ya wanaanga na mashabiki wa mambo ya anga wameshuhudia kuanza rasmi jukumu la darubini hiyo la kuchunguza anga la juu na kutafuta kama kuna maisha katika anga hiyo.
Mradi wa ujenzi wa darubini hiyo umeigharimu China kiasi cha dola za kimarekani milioni 180 na ulianza mwaka 2011, ikiwa ni miaka 17 baada ya kupendekezwa na wanaanga wa China.
Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwa wanasayansi, wahandisi, na wajenzi wa darubini hiyo mara ilipoanza rasmi kufanya kazi hii leo.