test

Jumatatu, 12 Septemba 2016

Chadema yatoa salamu za rambirambi


Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetoa salamu za pole kwa wananchi wote walioathirika na tetemeko la ardhi katika mikoa ya Kagera,Mwanza,Mara,Shinyanga na Tabora,tukio ambalo limesababisha vifo vya watu 16,kuharibu nyumba zaidi ya 840 na kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu.

  Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya habari wa chama hicho Tumaini Makene,chama hicho kimetoa wito kwa watanzania wote wanaoishi katika maeneo yaliyoathirika na tetemeko hillo na wengine kutoka nje ya eneo hilo kuwiwa kutoa misaada kwa waathirika wa tukio hilo katika wakati huu mgumu wakukabilliana na wakati huu mgumu.
  Amesema viongozi wa chama katika ngazi mbalimbali pamoja na wanachama wote wa Chadema wataungana na kusaidiana na waathirika kwa kila hali.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx