test

Jumamosi, 12 Septemba 2015

Urais 2015: Jaji Warioba amfananisha Magufuli na Nyerere




Aliyekuwa  Waziri Mkuu mstaafu wa Tanzania Jaji  Joseph Sinde Warioba amesema  kwamba Mgombea Urais wa CCM Dr. John Pombe Magufuli ni mtu muadilifu, Mchapakazi na Asiyekuwa na tamaa hivyo anazikaribia sifa za Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Akizungumza na wananchi  kwenye  mkutano wa kampeni uliofanyika juzi mjini Bunda,  Warioba alisema Dr. Magufuli ndiye anayestahili kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania kati ya wagombea nane kutoka vyama mbalimbali vilivosimamisha wagombea kwani mpaka kufika kwake hapo hakujatokana na fedha wala harufu ya fedha yeyote.

Alidai kuwa Vyama vya upinzani vilitakiwa kusimamisha wagombea wao wenyewe bila kuazima kutoka Chama cha Mapinduzi CCM jambo ambalo linawaondolea sifa za siasa zao za upinzani wa kweli nchini.

Install Application ya JUNGUKUULEO Uweze Pata Habari Kirahisi Zaidi

xxxxxxxxxxxxx

0 comments:

Chapisha Maoni