Miezi
michache iliyopita Abdul Kiba ambaye ni mdogo wake na AliKiba
alinukuliwa vibaya na vyombo vya habari kwamba yupo tayari kujiunga na
label ya ‘WCB’ ya Diamond kauli ambayo ilileta shida kwa mashabiki wa
AliKiba pamoja na team yake.
Muimbaji
huyo ambaye anafanya vizuri na video yake ya wimbo ‘Bayoyo’ ameiambia
Bongo5 kuwa kauli hiyo ilimfanya aonekane msaliti.
“AliKiba
alijisikia vibaya kwa sababu alijua kama ndo vile tena ndugu yake
nimekuwa msaliti kumbe ni watu walipata definition nyingine na ni kitu
ambacho hakiwezekani ila niliweza kufanya interviews nikaweka mambo
sawa,” alisema Abdul Kiba.
Akifafanua
kauli yake aliyozungumza na kutafsiriwa vibaya Abdul Kiba alisema “Siku
ambayo nilifanya interview walinielewa vibaya maongezi yangu, unajua
unaposikia kwamba kuna kazi hakuna kazi ya bure, kazi yoyote lazima iwe
na malipo, nilikubali kwamba kama WCB watanihitaji kwa kolabo au show
naweza nikajoin nao kufanya kazi ila sikutoa kauli kwamba naweza kwenda
label yao kwa sababu hata mimi na label yangu,”
Pia muimbaji huyo amewashukuru mashabiki wa team Kiba kwa kuendelea kuwasapoti wasanii wake pamoja na kazi zao.