Akiongea katika kipindi cha E-News cha East Africa TV, Witness amesema ameamua kufanya hivyo ili kuepuka kumsaliti mpenzi wake.
“Ukiweka tattoo sehemu kama niliyoweka mimi(kiunoni) inazuia, hata unapotaka kumsaliti mwenza wako yule unayekuwa naye inamnyima hamu kabisa na anashindwa hata kukutamani tena,” alisema Witness.
Pia Witness alisema kuwa watu wanadhani kuwa kuolewa ndiyo kumaliza kila kitu lakini kwa sehemu ambayo mapenzi yao yamefikia hakuna kitu ambacho anakihitaji tena kwakuwa mapenzi ni kuungana mkono na Ochu anamsaidia katika kila kitu anachofanya.