Waziri
Mkuu alitoa agizo hilo jana jioni (Jumapili, Agosti 07, 2016) wakati
alipozungumza na viongozi wa mikoa ya Mbeya, Katavi, Songwe, Rukwa,
Ruvuma, Iringa na Njombe mara baada ya kuwasili mkoani Mbeya kwa ajili
ya kufunga maadhimisho ya maonyesho ya nane nane kwa mikoa ya Kanda ya
Nyanda za Juu Kusini yanayofanyika mkoani Mbeya.
‘‘TRA
waendelee kukusanya mapato vizuri ila kuna wakusanya kodi wanaotaka
kuharibu mkakati wa Serikali kwa kufanya mambo ya hovyo kwa kuwaongezea
viwango vikubwa vya kodi kuliko kodi stahili wanavyotakiwa kulipa na
kufanya suala hili liwe kama tatizo au adhabu kwao jambo ambalo si
sahihi. Naagiza watendaji wa TRA wanaofanya hivyo wasakwe na wachukuliwe
hatua“, alisema.
‘‘Wafanyabiashara
mnaoonewa kwa chuki binafsi na watendaji wa TRA toeni taarifa ili
muweze kufanya biashara zenu kwa uhakika bila ya wasiwasi lengo ni
kuwafanya muweze kulipa kodi sahihi kwa mujibu wa sheria“, alisema.
Ili
kufanikisha mpango huo Waziri Mkuu amewaagiza wakuu wa mikoa na wilaya
kuwasikiliza wafanyabiashara ambao wana malalamiko ya kweli ya
kutotendewa haki katika kutozwa kodi kwa sababu mchango kupitia kodi ni
kwa ajili ya kuendeleza uchumi wa Taifa.
Katika
hatua nyingine ameitaka idara ya Uhamiaji ijikite katika kudhibiti
watumishi wasiokuwa waaminifu ambao wamekuwa wakichukua rushwa kutoka
kwa wageni wanaotoka nje ya nchi na kuwaingiza nchini bila ya kuwa na
vibali maalumu.
‘‘Ni
lazima tuhakikishe hakuna uingiaji holela ndani ya nchi na hasa kwa
wanaoingia bila vibali maalumu kwani bila ya kudhibiti suala hilo
tunaacha mianya ya kuingia watu wasiokuwa na nia njema na Taifa letu.
Watu watakaobainika wameingia nchini bila ya vibali wakamatwe na
kufikishwa katika vyombo vya sheria,“ alisema.
Alisema
kitendo cha mipaka kushindwa kudhibitiwa na kuruhusu uingiaji holela wa
watu wasiokuwa na vibali chini kunasababisha Serikali kushindwa
kuteleza ipasavyo mipango yake ya kuwahudumia wananchi kulingana na
idadi halisi.
Mbali
na kuiagiza Idara ya Uhamiaji pia Waziri Mkuu alisema wakuu wa mikoa ya
mipakani wana jukumu la ziada la kuhakikisha wanadhibiti mipaka yote na
kuhakikisha hakuna watu wanaoingia nchini bila ya kuwa na vibali.
Hata
hivyo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa mikoa kote nchini kuendelea
kuimarisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo yao na kuhakikisha
nchi inaendelea kuwa na amani na utulivu ili Watanzania waweze
kutekeleza shughuli zao za maendeleo kama walivyojipangia.
“Natambua
kuwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ndio wenyeviti wa kamati za
ulinzi na usalama katika maeneo yenu, endeleeni kuimarisha hali ya
ulinzi na usalama. Nchi hii tunahitaji iwe tulivu na salama na ni
wajibu wenu kuhakikisha kwamba lolote linalotokea mnalikabili vilivyo“, alisema.
Awali
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mhe. Makalla alipokuwa akisoma taarifa ya mkoa
huo kwa Waziri Mkuu alisema mkoa huo una jumla ya viwanda 1,653 kati
yake vikubwa ni tisa, vya kati 19 na vidogo 1,625 na bado wanaendelea
kuzisimamia halmashauri kutenga maeneo zaidi kwa ajili ya kuongeza na
kupanua viwanda.
Mhe.
Makalla alisema katika eneo hilo la viwanda mkoa una kiwanda kimoja cha
kusindika nyama cha Tanganyika Pachers kilichopo wilayani Mbeya ambacho
hakijawahi kufanya kazi tangu kilipojengwa na kufungwa mitambo mwaka
1975.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema usimamizi wa kiwanda hicho uko chini ya Masajili
wa Hazina na kwamba tayari kuna muwekezaji amepatikana kwa ajili ya
kukiendesha hivyo ameiomba Serikali kuharakisha taratibu za mikataba ili
kiweze kuanza kufanya kazi.