Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo vilivyotolewa na kampuni ya Vodacom Tanzania kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaopokea ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wengine pichani ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (kulia) na Gerald Hando.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Matina Nkurlu (kushoto) akionyesha moja ya T-shirt wakati kampuni ya Vodacom Tanzania ilipokabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa ajili ya tamasha la Mziki Mnene litakaloanza kufanyika katika mikoa ya Pwani na Dar es Salaam mwishoni mwa wiki hii. Wanaoangalia ni waratibu wa tamasha hilo litakaloendeshwa na kituo cha redio cha Efm, Dennis Busulwa maarufu Ssebo (katikati) na Gerald Hando.
KATIKA juhudi za kuendeleza sekta ya michezo nchini,Kampuni ya mawasiliano ya Vodacom Tanzania leo imekabidhi jezi za michezo kwa Uongozi wa Tamasha la Mziki Mnene na Vodacom ulioandaa tamasha mahusisi kwa timu mbalimbali zitakazoshiriki katika mpira wa miguu wa maveterani katika tamasha hilo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani wakati wa tamasha hilo lililoandaliwana kituo cha EFM linalotarajiwa kuzinduliwa Jumamosi ijayo chini ya udhamini wa Vodacom Tanzania.
Akiongea katika hafla ya kukabidhi kwa uongozi huo,Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu alisema Vodacom Tanzania inafurahi kudhamini tukio hili muhimu lenye lengo la kutoa burudani kwa jamii kupitia tasnia ya muziki na michezo.
“Vodacom tunafurahi kushiriki katika tukio hili la kuleta burudani kwenye jamii na ndio maana kampuni imekuwa mstari wa mbele kudhamini michezo na Sanaa kwa kuwa inaamini kupitia sekta ya michezo watanzania wengi wanaweza kupata burudani wazipendazo na kupumzisha akili pia kupitia tamasha hili wananchi watapata fursa ya kupata na kununua bidhaa mbalimbali za mawasiliano kutoka Vodacom popotelitakalofanyika tamasha hili huduma zetu zitakuwepo na tutaendelea kudhamini matukio ya burudani kwa ajili ya kuinua vipaji vya Sanaa na michezo kama ambavyo kwa sasa tunavyoendelea kudhamini ligi kuu ya soka ya Tanzania bara na mashindano ya kucheza muziki wa dansi ya Dance 100% na tuzo za wasanii ya EATV”Alisema.
Akiongea baada ya kupokea vifaa hivyo vya michezo Mratibu wa tamasha hilo,Denis Sebbo amesema kuwa tamasha la muziki mnene mwaka huu, litafanyika kwa kipindi cha muda wa wiki 12 ambapo muziki utapigwa katika baa 12 za Jijini Dar es salaam na Mkoa wa Pwani.
Baadhi ya wasanii ambao watapamba tamasha hilo aliwataka kuwa ni Machupa,Msaga Sumu,Dula Makabila,Easy Man,Khalid Chokoraa,Mc KKoba,Shoz Dear,Peter Msechu,AT,Majid Migoma, Dogo Niga na Rublay.
Alisema tamasha la muziki mnene mwaka huu litaenda sanjari na kampeni ya NJE NDANI ambapo vipindi vinne mbalimbali vya redio hiyo viratushwa live naaliwataka wapenzi wa michezo na burudani kuhudhuria tamasha hili ambalo ni mwisho wa burudani na tayari limeishaanza kuwa gumzo ya jiji.