Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Prof Joyce Ndalichako amesema
wizara hiyo imelazimika kusitisha malipo ya fedha za mafunzo kwa vitendo
kwa wanafunzi wa elimu ya juu kwa muda wa wiki mbili ili kupisha zoezi
la uhakiki wa wanafunzi hewa
Amesema
hadi sasa wanafunzi hewa zaidi ya 2000 tayari wamebainika kwenye vyuo
mbalimbali nchini na walikuwa tayari kupokea fedha hizo jambo ambalo ni
hasara kwa serikali.
Prof.
Ndalichako amesema, tayari amewaagiza wakuu wote wa vyuo kuwasilisha
upya majina ya wanafunzi wanaostahili kupatiwa fedha hizo bila
udanganyifu.
Amefafanua
kwamba, wamegundua taarifa zilizopelekwa awali zilikuwa na udanganyifu
hivyo serikali imelazimika kusitisha zoezi la upelekaji fedha kwenye
vyuo hivyo.
Kwa
upande wa wanafunzi ambao vyuo vyao vimefungiwa Prof. Ndalichako
amesema tayari wametoa maelekezo ya kuwasaidia kupata haki yao muhimu ya
kusoma na kusisitiza hakuna mwanafunzi hata mmoja ambaye atakosa msaada
wa serikali