Serikali imewatoa hofu wahitimu wa vyuo mbalimbali nchini kuwa itaanza zoezi la kuajiri punde tu itakapokalimisha zoezi la uhakiki watumishi hewa nchini.
Waziri wa ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora Bi Angela Kairuki
Waziri wa nchi ofisi ya rais menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, Angela Kairuki amesema hayo kwenye kipindi cha ‘TUNATEKELEZA’ kinachorushwa na TBC 1 ambapo amebainisha kuwa jumla ya ajira elfu 71 zinatarajiwa kutangazwa katika kipindi cha mwaka huu wa fedha.
“Ukiangalia katika mwaka huu wa fedha ajira ambazo tunatarajia kuzitoa katika serikali ni takribani elfu 71 na 496 hatujafuta ajira hizo ni lini tu mchakato huo unaanza ndicho ambacho tumekuwa tumekiahirisha kwa muda mfupi na nipende kuwatia moyo kuwa waendelee kusubiri wasijiinge katika makundi ambayo hawastahili kuingizwa waendelee kuwa na uadilifu na muda si mrefu wataingia katika utumishi wa umma”, alisema Kairuki.
Akizungumzia suala la watumishi hewa, Waziri Kairuki alisema serikali imebaini watumishi 16,127 baada ya kufanya zoezi la kuhakiki katika idara na taasisi zake zote nchini kuanzia mwezi March hadi Augusti mwaka huu.
“Tunasubiri kwa kiasi kikubwa ilikuwa ni tathmini ya mwisho kutoka kwa wale waajiri ili waweze kutueleza kabisa kama watumishi walioondolewa ni wangapi sisi tunayo takwimu ya 16,127 lakini inawezekana kuna taasisi nyingine amekwambia ana mia moja kumbe ana tisini tu kwahiyo ilikuwa ni lazima tufanye uhakiki na ninavyoongea sasa hivi timu yangu ikiongozwa na katibu mkuu tayari inazunguka atika mikoa mbali mbali. Baada ya kupata takwimu hiyo tutapeleka kwa mheshimiwa rais halafu taratibu zingine zitaendelea”,aliongezea.